Wednesday, September 26, 2012

WAKALA WA USAMBAZAJI UMEME VIJIJINI (REA) KUENDESHA SHINDANO LA KUSAMBAZA UMEME. Shule na Hospitali vijijini kunufaika.

Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Umeme Vijijini (REA) Lutengano Mwakahesya (PhD) akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusu kuanza kwa shindano la usambazaji wa umeme vijijini, ambapo taasisi mbalimbali za vijijini ziliwasilisha maombi yao, ambapo mchujo wa shindano hilo unatarajiwa kufanyika Mkoani Arusha Oktoba 1 na 2. Mradi huo ni wa ushirikiano kati ya Serikali na Benki ya Dunia (WB), kulia ni Mkurugenzi wa fedha wa REA George Nchwali.



Baadhi ya wafanyakazi wa REA wakifuatilia mkutano huo kati ya waandishi wa habari na Mkurugenzi wa wakala huyo.

No comments:

Post a Comment