Wednesday, September 26, 2012

DJ Nijo Kukamua Sun Ciro, Nyumbani Lounge

Kipindi maarufu cha “Hyped East Africa Show” kinachorusha na kupitia kingamuzi cha Zuku Pay TV, wiki hii kinatarajia kumleta DJ Nijo kupiga shoo kali kwenye kumbi maarufu jijini Dar es Salam. 

Dj Nijo na msaidizi wake Dada Amani wanatarajiwa Dares Salaam Alhamisi ya wiki hii. Akizungumza na waandishi wa habari, mmoja wa waratibu wa ujio huo, hapa nchini Shella Njeri, alisema kuwa DJ Nijo atapama kumbi mbili maarufu za Sun Ciro na Nyumbani Lounge kwa kupiga shoo ya aina yae ambapo pia kutakuwa na zuria maalumu la wangeni and watu maarufu kupita humo.

 “Ijuma hii ya Septemba 28, atwasha mota pale Sun Ciro, na siku inayofuata, Jumamosi, atamalizia shoo nyingine kwenye ukumbi wa Nyumbani Lounge, alisema Shella. 

 Pia aliendelea kusema kuwa kweny shoo hizo, kutapambwa na ubora wa hali ya juu na wengi watasuuzika kwa kushuhudia shoo hiyo ambayo imekuwa ikiacha gumzo kila jiji anazopiga shoo DJ Nijo zikiwemo ndani ya Afrika Mashariki.



DJ Nijo yuko kwenye ziara ya kupiga shoo kwenye klabu maarufu za miji mikubwa ndani ya Afrika Mashariki na vipindi vyote vya Hyped East Africa vinarushwa Zuku Afrika kila jumamosi saa 3:30 usiku. Shoo ya “Hyped East Africa” imefanywa katika miji ya Malindi, Embu, Nairobi, Nyeri, Eldoret, Kisumu, Embu, na hivi karibuni vilabu vya ‘Anje Noir’ na ‘Cayenne’ jijini Kampala.

No comments:

Post a Comment