HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, September 28, 2012

Ufunguzi wa Tamasha la Muziki wa Dansi nchini lafana sana Viwanja vya Leaders Club usiku huu

 Wanamuziki wakongwe wa bendi ya Muziki wa Dansi hapa nchini ya Msondo Ngoma (Baba ya Muziki) wakikamua vilivyo katika Ufunguzi wa Tamasha la wazi la Muziki wa Dansi Tanzania linaloendelea kufanyika usiku huu katika viwanja vya Leaders Club,jijini Dar es Salaam.Tamasha hili ambalo ni la kipekee katika tasnia hii ya Muziki wa Dansi,litafanyika kwa siku mbili mfululizo ikiwa leo ndio siku yake ya kwanza.
 Wapulizaji wa Midomo ya Bata (Trampet na Sexaphone) wa Bendi ya Msondo Ngoma wakiongozwa na Roman Mng'ande a.k.a Romario (kulia) wakifanya vitu vyao katika Tamasha hilo usiku huu.
 Roman Mng'ande akifanya vitu vyake wakati Bendi yao ikitumbuiza kwenye Tamasha hilo usiku huu.
 Kundi zima la Bendi ya Muziki ya Mashujaa wakiongozwa na Charles Baba (pili kushoto) wakikamua vilivyo kwenye Tamasha la wazi la Muziki wa Dansi hapa nchini linaloendelea hivi sasa katika viwanja vya Leaders Club,jijini Dar es Salaam usiku huu.
 Rapa wa Mashujaa akiongoza safu ya Mashambulizi kwa Bendi yake.
 Mkaanga Chips (Mpiga Drums) wa Mashujaa Band kazini.
 MCD akiendelea na libeneke lake la Kusakata Tumba ndani ya Mashujaa Band kwenye Tamasha la Wazi la Muziki wa Dansi hapa nchini linaloendelea kufanyika hivi sasa katika viwanja vya Leaders Club,jijini Dar es Salaam.
 Kiongozi wa Madansa wa Kiume wa Bendi ya Mashujaa akionyesha kogo zake kwenye Tamasha hilo usiku huu.
  Timu nzima ya Mashujaa Band Stejini.
 Mc wa Tamasha hilo,Ben Kinyaiya akiwa na Mkonge wa Muziki wa Dansi hapa nchini,Mzee Muhidin Gurumo.
Hapa akiwa na Blogger Machachari wa Libeneke la Bofya hapa utaliona,Mzee John Kitime.

3 comments:

  1. Tamasha hili ni la bendi mbili tu??mbona hizi picha naona.....tu??

    ReplyDelete
  2. Wee Anonymous September 28,2012 11:53 PM.kama unataka kuona bendi zingine nenda viwanja vya lidaz klabu na sio unataka kuonyesha ujuaji wako kwa mzee kwa Mtaa kwa Mtaa alietuletea taswira hizi mwanana.

    ReplyDelete
  3. Nimebahatika kupita pale usiku wa leo,lakini tamasha lenyewe limepwaya kama nini kwa kukosa idadi kubwa ya watu.

    ReplyDelete

Post Bottom Ad