Mfanyakazi
katika Kiwanda cha Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Adolf Ndyeabura
(aliyevalia fulana ya Yanga kulia) akiwaonyesha kocha wa timu ya Yanga,
Thom Sainfiet, na baadhi ya wachezaji wa timu hiyo jinsi bia
zinavyopikwa juzi Alhamisi wakati timu hiyo yenye maskani yake katika
mtaa wa Jangwani jijini, ilipofanya ziara yake katika kiwanda cha TBL
kilichopo Ilala jijini Dar es Salaam.
Meneja
wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager, George Kavishe (kushoto) akiwa na
beki mpya wa timu ya Yanga, Mbuyu Twite (katikati) na Msemaji wa timu
hiyo, Louis Sendeu Alhamisi wakati timu hiyo yenye maskani yake katika
Mtaa wa Jangwani jijini Dar es Salaam ilipofanya ziara katika kiwanda
cha kampuni ya Bia Tanzania (TBL). Anayeonekana nyuma yao ni kocha wa
timu hiyo, Thom Sainfiet.
Meneja
wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager, George Kavishe (kushoto kabisa)
akiwa na baadhi ya viongozi wa vitengo mbalimbali vya Kampuni ya Bia
Tanzania (TBL) pamoja na wachezaji, benchi la ufundi na viongozi wa timu
ya Yanga juzi Alhamisi wakati mabigwa hao wa Kombe la Kagame
walipotembelea kiwanda cha TBL kilichopi Ilala jijini Dar es Salaam.
Wachezaji
wa timu ya Yanga pamoja na benchi la ufundi la timu hiyo na baadhi ya
viongozi wa timu wakiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wanawake
katika Kiwanda cha Bia Tanzania (TBL) juzi Alhamisi wakati timu hiyo
ilipofanya ziara kiwandani hapo jijini Dar es Salaam.



No comments:
Post a Comment