Mkufunzi wa warembo katika shoo ya Redd's Miss Temeke, Dickson Daud akiwanoa warembo hao katika Club ya TCC Chang'ombe jana, tayari kwa shindano lao litakalofanyika Septemba 21 mwaka huu.
Warembo wa Redd's Miss Temeke, wakiwa mazoezini jana katika Club ya TCC
Chang'ombe , tayari kwa shindano lao litakalofanyika Septemba 21 mwaka huu.
VIMWANA 15 wa Redd's Miss Temeke, juzi wameanza rasmi kambi yao katika Club ya TCC Chang'ombe tayari wa kinyang'anyiro cha kanda hiyo, kumrithi mremboHusna Twalib anayeshikilia taji hilo. Warembo hao ambao wameanza programu ya shoo kwa wiki hii, chini ya ukufunziwa Dickson Daud kutoka kikundi cha THT, wanatoka katika vitongoji vya Kigamboni, Kurasini na Chang'ombe ambapo kila sehemu wametoka warembo watanoambapo washindi watatu wa kwanza watapata fursa ya moja kwa moja kushiriki Redds Miss Tanzania 2012. Warembo hao ni Agness Goodluck, Angela Gasper, Flaviana Maeda,Edna Sylvester, Catherine Masumbigana, Khadija Kombo, Neema Doreen, Flora Kazungu, LilianJoseph, Elizabeth Peter, Elizabeth Boniphace, Jesca Haule, Zulfa Bundala, MariamNtakisivya na Esther Albert. Temeke imewahi kutwaa taji la Miss Tanzania mara tatu, kupitia waremboHappiness Sosthenes Magesse aka Millen mwaka 2001, Sylvia Remmy Bahammwaka 2003 na Genevieve Mpangala. Lakini pia imetoa warembo waliowahi kushika nafasi ya pili na tano bora katika Miss Tanzania kama Jokate Mwegelo, IreneUwoya, Irene Kiwia, Queen David, Cecylia Assey, Sabrina Slim, Miriam Odemba,Ediltruda Kalikawe na Asela Magaka.Mbali ya Redd's, Miss Temeke 2012 pia imedhaminiwa na Dodoma Wine, gazeti laJambo Leo, Push Mobile, City Sports Lounge, 100.5 Times FM, Kitwe GeneralTraders na 88.4 Clouds FM. Warembo wanaendelea na mazoezi na leo, Agosti 5wanatarajia kutembelewa na Miss Tanzania 2010, Genevieve Mpangala ambaye pia ni MissTemeke wa mwaka huo.

No comments:
Post a Comment