HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, September 5, 2012

Mkutano wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi ya Kusini mwa Afrika (SADC TROIKA)

 Rais Jakaya Kikwete akimpokea  Rais Hifikepunye Pohamba wa Namibia  Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere akiwa na mwenyeji wake Rais Jakaya Kikwete.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Bernard Membe akimlaki Waziri wa Ulinzi na Veterani wa Jeshi wa  Afrika Kusini Bi. Nosiviwe Mapisa-Nqakula.
Rais Jakaya Kikwete akimpokea Rais Hifikepunye Pohamba wa Namibia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere akiwa na mwenyeji wake Rais Jakaya Kikwete.
Rais Joseph Kabila akipeana mikono na Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es salaam Bw. Suleiman Kova wakati alipowasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere akiwa na mwenyeji wake Rais Jakaya Kikwete. Rais Kabila alihudhuria mkutano huo kama mgeni mwalikwa.
Mwenyekiti wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi ya Kusini mwa Afrika(SADC TROIKA) Rais Jakaya Kikwete akiongea na wanbahabri mara baada ya kumalizika kikao cha siku moja cha asasi hiyo katika hoteli ya Kilimanjaro Hyatt Regency jijini Dar es salaam. Kushoto ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Bernard Membe na kulia ni Katibu Mtendaji wa SADC Dkt Tomaz A. Salomao.
Mwenyekiti wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi ya Kusini mwa Afrika(SADC TROIKA) Rais Jakaya Kikwete akifungua kikao cha siku moja cha asasi hiyo katika hoteli ya Kilimanjaro Hyatt Regency jijini Dar es salaam. Kushoto ni Mwenyekiti wa SADC Rais Armando Emílio Guebuza wa Msumbiji na kati ni Katibu Mtendaji wa SADC Dkt Tomaz A. Salomao.
Katibu Mtendaji wa SADC Dkt Tomaz A. Salomao akitoa maelezo kabla ya kuanza kikao.
Kuanza kwa kikao cha Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi ya Kusini mwa Afrika(SADC TROIKA).
Mwenyekiti wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi ya Kusini mwa Afrika(SADC TROIKA) Rais Jakaya Kikwete akiongea na wanbahabri mara baada ya kumalizika kikao cha siku moja cha asasi hiyo katika hoteli ya Kilimanjaro Hyatt Regency jijini Dar es salaam.
Maofisa wakimsikiliza Mwenyekiti wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi ya Kusini mwa Afrika(SADC TROIKA) Rais Jakaya Kikwete akifungua kikao cha siku moja cha asasi hiyo katika hoteli ya Kilimanjaro Hyatt Regency jijini Dar es salaam
Mwenyekiti wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi ya Kusini mwa Afrika(SADC TROIKA) Rais Jakaya Kikwete akiwa na wageni wake wakielekea kwenye kikao cha siku moja cha asasi hiyo katika hoteli ya Kilimanjaro Hyatt Regency jijini Dar es salaam. Kutoka kushoto ni Rais Hifikepunye Pohamba wa Namibia, Rais Kikwete, Rais Armando Emílio Guebuza wa Msumbiji na Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
Mwenyekiti wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi ya Kusini mwa Afrika(SADC TROIKA) Rais Jakaya Kikwete akiwa na wageni wake wakielekea kabla ya kikao cha siku moja cha asasi hiyo katika hoteli ya Kilimanjaro Hyatt Regency jijini Dar es salaam. Kutoka kushoto ni Rais Armando Emílio Guebuza wa Msumbiji, Rais Hifikepunye Pohamba wa Namibia, Rais Kikwete, na Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).PICHA NA IKULU


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad