HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, September 25, 2012

Mama Salma Kikwete katika mkutano wa wake wa viiongozi wa Afrika, New York, Marekani


 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akizungumza wakati wa majadiliano ya kubadilishana mawazo kuhusu  namna ya  kuwasaidia na kuwahamasisha  wanafunzi   kushirikia katika masomo ya  Sayansi, Tekinolojia, Uhandisi na  Hesabu Mkutano huo ambapo  uliandaliwa na Bi Savannah Maziya Mkurugenzi  Mtendaji wa Bunengi Gropu kwa kushirikiana na Makampuni mengine na kupewa jina la  la African First Ladies Roundtable, Umefanyika katika ukumbi wa mikutano wa jengo la  Suisse America , jijini New York na kuhudhuriwa na  baadhi ya  wake wa marais,  wakurugenzi wa makampuni mbalimbali, wanadiplomasia na wahadhiri.
Mama Salma Kikwete akibadilishana mawazo na   Bibi Katalin Bogyay Balozi wa  Hungary UNESCO na amebobea katika diplomasia ya utamaduni  na mtetezi mkubwa wa masuala yahusuyo  fursa sawa ya elimu kwa mtoto wa kike.
 Mama Salma Kikwete akiwa na Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe Mwanaidi Sinare Maajar, Balozi wa Umoja wa Afrika katika Umoja wa Mataifa Mhe. Amina Salum Ali na Mshauri wa Rais  mambo ya Diplomasia Balozi Liberata Mulamula kabla ya kuhudhuria mkutano wa  African First Ladies Roundtable jijini New York, Marekani, leo.
 Mama Salma Kikwete akihudhuria mkutano huo  Kwa habari na picha zaidi BOFYA HAPA

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad