Mkurugenzi
wa Taasisi isiyo ya kiserikali ya TAYODA, Jackson Kangoye, akikata mti
kwa ajili ya kuandaa shamba katika kijiji cha Msagali, Mpwapwa mkoani
Dodoma, juzi, taasisi hiyo inajihusisha na umahasishaji wa vijana
kuingia kwenye kilimo badala ya kutegemea ajira serikalini.
Wananchi
wa kijiji cha Msagali, Mpwapwa mkoani Dodoma, wakimsikiliza Mkurugenzi
Mtendaji wa Taasisi isiyo ya kiserikali ya TAYODA, Jackson Kangoye,
hayipo pichani alipokuwa akizungumza nao juzi na kuwahamasisha
kujiingiza kwenye kilimo.
Vijana
wa kijiji cha Kibakwe, Mpwapwa mkoani Dodoma, wakianda shamba kwa ajili
ya kuanza kulima. Vijana hao wamehamasishwa na taasisi isiyo ya
kiserikali ya TAYODA kujiingiza kwenye kilimo badala ya kusubiri
kuajiriwa.
Na mwandishi wetu
TAASISI
ya Tanzania Youth Development Agenda (TAYODA), imesema mchakato wake wa
kuanzisha benki ya vijana kwa lengo la kuwakomboa na kupata mikopo
kupitia benki hiyo, unaendelea na upo kwenye hatua nzuri.
Mkurugenzi
Mtendaji wa TAYODA, Jackson Kangoye, alisema hayo juzi wakati
akizungumza na baadhi ya vikundi vya vijana wilayani Mpwapwa, Dodoma
ambao wamekuwa wakiwezeshwa na taasisi hiyo kufanya shughuli za kilimo
na ufugaji.
Alisema
taaratibu za kuanzisha benki hiyo zimeanza na wameshafikia hatua mzuri
na wanasubiri hatua za kitaalamu kuanza maandalizi ya kuifungua.
Kangoye, ambaye pia ni mgombea wa nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa UVCCM
Bara.
alisema
lengo la kuanzishwa benki hiyo ni kwa ajili ya kuwawezesha vijana
kupata mikopo kupitia benki yao badala ya kutumia benki zingine. "Vijana
wenzangu, taasisi yetu iko mbioni kuanzisha benki ya vijana, itakuwa
mahususi kwetu na hivi sasa tumekutana na wataalamu wa masuala ya
kibenki ambao watatushauri jinsi ya kuiendesha," alisema.
Alisema
baada ya kupata ushauri kutoka kwa wataalamu wa masuala ya kibenki,
watakutana na baadhi ya vijana kuangali namna ya kuiendesha benki hiyo.
Kwa upande wao baadhi ya vijana, walisema wamefurahishwa na uamuzi huo
na wamewaomba viongozi wa taasisi hiyo kuhakikisha benki hiyo
inafunguliwa kwa wakati.
Said
Husein, mkazi wa Kibakwe, alisema kuanzishwa kwa benki hiyo
kutawakomboa vijana wengi ambao watakuwa wakipata mikopo kupitia benki
hiyo.

No comments:
Post a Comment