Mwnyekiti wa MISA TAN Mohamed Tibanyendera, akizungumza
na waandsihi wa habari kuhusu hatua wanazozichukua dhidi ya Serikali kutokana
na kulifungia gazeti la Mwanahalisi.
Mwenyekiti wa kamati ndogo ya asasi za kiraia inayoshughulikia
harakati za kulifungulia gazeti la MwanahalisiMarcossy Albanie akizungumza na
waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo.
Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa kazini kuhakikisha
wanapata kila tukio.
KAMATI
ndogo iliyoundwa na taasisi nne za kiraia nchini ambayo inaratibu mchakati wa
kupigania haki ya kufunguliwa kwa gazeti la Mwanahalisi leo imeipa serikali
siku saba kuliruhusu gazeti hilo kuendelea kuchapishwa.
Akizungumza
mbele ya waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Mwenyekiti wa kamati hiyo
Marcossy Albanie, amesema hawana sababu yakwenda mahakamani juu ya jambo hilo
kwasababu hata serikali haikutumia njia hiyo ya mahakamani kwani ilikuwepo
badalayake wametumia sheria kandamizi ya vyombo vya habari inayopigiwa kelele
na wadau wa habari.
Kamati
hiyo inayoungwa mkono na taasisi tano za kiraia baadhi ya taasisi hizo ni MISA
TANZANIA, TANZANIA HUMANRIGHTS DEFENDERS COALITIONS NA KITUO CHA SHERIA NA HAKI
ZA BINADAMU (LHRC) imeitaka serikalikutekeleza madai yafuatayo.
1.Kuitaka
serikali kulifungulia gazeti la Mwanahalisi maramoja.
2.Serikali
badala ya kushughulikia Watetezi wa haki na wanahabari wanaofichua uovu
ishughulike na wahalifu waluiomteka Dk.Ulimboka.
3.
Serikali iache kabisa na ukandamizaji huu wa haki na uhuru wa habari.
WAANDISHI
WA HABARI WAOMBWA YAFUATAYO SERIKALI ISIPO TEKELEZA HAYO:
Kutochapisha
habari yeyote itakayo wahusu Waziri wa habari wa Wizara hiyo na Naibu wake,
Katibu Mkuu wa Wizara hiyo na Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo.
Kusimama
kidete kuunga mkono harakati hizo hadi zinapata ufumbuzi wake.
Ikumbukwe
kesi Na.34/2009 iliyofunguliwa tangu 2008 kupinga sheria ya magazeti ya 1976
iliyotumika kufungia Mwana Halisi haijasikilizwa mpaka sasa.
Mwisho:

No comments:
Post a Comment