HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, August 16, 2012

Rais Shein akutana na kuzungumza na Wananchi wa Marumbi Wilaya ya Kati,kisiwani Pemba


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Viongozi alipowasili katika viwanja vya Skuli ya Sekondari ya Marumbi Kuzungumza na Wananchi na Wavuvi katika kijiji hicho leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, alipokuwa akizungumza na na Viongozi na wananchi pamoja na Wavuvi wa Kijiji cha Marumbu Wilaya ya Kati Mkoa Kusini Unguja leo,katika Skuli ya Sekondari ya Marumbi,kuhusu tatizi la Mzozo wa Wavuvi wa kijiji hicho kuchukuliwa Boti zao na Wavuvi wa Kijiji cha Chwaka na hatimae kuzichoma Moto boti hizo.
Waziri wa Uvuvi na Mifugo Abdilah Jihadi Hassan,akitoa maelezo mbele ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,wakati alipofika katika Skuli ya Marumbi kusikiliza malalamiko ya mzozo wa Wananchi wa Kijiji cha Marumbi na Wananchi wa Chwaka, badala ya Chwaka walipozichukua Boti mbili na Kuzichoma Moto hivi karibuni.
Naibu Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano Issa Haji Gavu,akitoa maelezo mbele ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,wakati alipofika katika Skuli ya Marumbi kusikiliza malalamiko ya mzozo wa Wananchi wa Kijiji cha Marumbi na Wananchi wa Chwaka, badala ya Chwaka walipozichukua Boti mbili na Kuzichoma Moto hivi karibuni.
Akina mama wa Kijiji cha Marumbi Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein ,alipofika Skuli ya Sekondari ya Marumbi Kuzungumza na Wananchi na Wavuvi katika kijiji hicho leo,kusikiliza kilio chao cha kuchomewa Boti zao mbili.Picha na Ramadhan Othman,Ikulu ZNZ.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad