HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, August 13, 2012

Rais Kikwete awasili kutoka Ghana, afuturu na watoto Yatima na Walemavu ikulu

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Said Meck Sadik muda mfupi baada ya kuwasili akitokea nchini Ghana ambapo alishiriki mazishi ya aliyekuwa Rais wan chi hiyo Marehemu John Atta Mills.Kushoto ni Mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama Jenerali Davis Mwamnyange.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisoma barua aliyoandikiwa na mtoto Khaitham Jumbe(kulia) wakati wa futari aliyowaandalia watoto walemavu na yatima ikulu jijini Dar es Salaam.Katikati anayeangalia ni mtoto Hamida Jacks mdogo wake Khaitham.Mtoto Khaitham Jumbe ni mlemavu wa ngozi na alikuja ikulu na wazazi wake.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na Mkewe Mama Salma Kikwete wakigawa zawadi kwa watoto yatima na walemavu walohudhuria futari waliyowaandalia ikulu jijini Dar es Salaam jana jioni.
Baadhi ya watoto yatima na walemavu wakishiriki katika futari ikulu jijini Dar es Salaam jana jioni(picha na Freddy Maro).

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad