Mahmoud Ahmad,Arusha
Katibu mkuu wa wizara ya Mawasiliano sayansi na teknolojia Florence Turuka amesema kuwa shirika la posta lipo katika mkakati wa kuboresha huduma zake ili kuongeza tija na ufanisi na kuendana na teknolojia iliyopo ya mawasiliano.
Aliyasema hayo wakati akifungua semina ya siku tatu inayozishirikisha nchi 20 za kiafrika zinazozungumza kiingereza unafanyika jijini hapa na kubainisha kuwa mifumo ya kiutendaji kazi ya shirika hilo inatakiwa kuendana na ulimwengu wa utandawazi na kuwa shirika la posta limeandaa mpango wa muda mrefu katika kuendesha shughuli zake.
Turuka alisema kuwa shirika la posta lina mikakati ya kuanzisha huduma mpya zinazokwenda na wakati sanjari na kuanzisha huduma ya anwani ya makazi na kwa kuanzia mikoa ya Arusha na Dodoma ilikuwapa urahisi watanzania kupata huduma pale walipo na kwa wakati.
“Tunatarajia kunganisha huduma za zamani, haduma za fedha na huduma za kielektroniki ili kuweza kufikia malengo ya ukusanyaji wa fedha na jinsi ya matumizi yaliyosahihi”alisema Turuka.
Nae Postamaster Mkuu wa shirika la Posta Deusikhamisi Mndeme alisema kuwa shirika la posta limejipanga kuwafikishia wananchi huduma zake pale walipo na kuweza kufanyabiashara nao sehemu yeyote kwa kutumia mtandao wa kompyuta naye mteja kupata huduma hiyo kwa wakati.
Mndeme alisema kuwa kwa sasa siunaona teyari huduma za mawasiliano zilivyoboreshwa mahitaji yote unayapata kwa njia ya mtandao hivyo nasi tunajipanga kufika huko na kwa kuanzia kwa kuapata uzoefu kutoka kwa wenzetu na mashirika ya kimataifa kupitia semiana hii.
Mndeme alibainisha kuwa shirika limejipanga kufanyakazi kwa tija na kuandaa matumizi sahihi ya fedha na makusanyo kama mataifa yaliyoendelea na mpango huo ni wa muda mrefu katika.

.jpg)
No comments:
Post a Comment