Leo ni Siku ya HEPI BESDEI ya kuzaliwa Ankal Issa Michuzi. Naye kaamua kusherehekea kimyakimya ili kuruhusu ndugu, jamaa na marafiki pamoja na wadau wafanye hivyo kwa niaba yake. Anamshukuru Muumba wa Vyote kwa kumjaalia umri huu na kumpa afya njema.
Ujumbe wake kwa wote ni ule ule kwamba Usichague na wala usibague maana atayekuzika humjui. Pia si rahisi kufurahisha kila mtu, cha muhimu ni kudumisha amani na upendo hata pale mnaposigana kimawazo. Si vyema kumlazimisha mtu apende upendacho ama achukie ukichukiacho kwani dunia haikuuumbwa hivyo. Mwenye macho na asikie...


No comments:
Post a Comment