HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, July 6, 2012

WAJUMBE WA BODI YA WAKURUGEZNI NSSF WATEMBELEA MAONYESHO YA SABASABA

 Ofisa wa NSSF, Pilly Mpenda akimkaribisha Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa NSSF, Abubakar Rajabu katika banda la Shirika la Taifa la Hifahi ya Jamii.
Ofisa wa Elimu kwa Umma wa NSSF, Alice Simba akitoa elimu kwa wanachama waliofika katika banda la Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) waliopotembelea banda la NSSF.
 Mkuu wa Uhusiano na Hudumna kwa Wateja wa NSSF, Eunice Chiume akitoa maelekezo kwa Wajumbe wa Bodi ya wakurugenzi walipotembelea Maonyesho ya 36 ya Biashara ya Kimataifa Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam
 Ofisa Mwandamizi wa NSSF, Julius Kisingi akitoa maelezo kuhusu mafao ya bima kwai Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa NSSF walipotembelea hilo.
 Ofisa Mipango Mkuu wa NSSF, Gerald Peter Sondo akifafanua jambo miradi ya ujenzi wa nyumba za bei nafuu wakati Bodi ya Wakurugenzi ilipotembelea banda la NSSF. Katikati ni Mwenyekiti wa Bodi, Abubakar Rajabu.
 Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Dk Ramadhani Dau akipeana mkono na Bernadeta Kaiza ambaye alifika katika banda la NSSF kutoa ushuhuda wake pamoja na kuishukuru NSSF kwa kugharamia  safari ya kusafirisha mwili wa marehemu mume wake ambaye alikuwa mwanachama wa NSSF WESTEDI aliyefariki nchini ns kusafirishwa na Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), kutoka marekani mpaka Tanzania kwa ajili ya mazishi. 
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) akizungumza na Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi walipofka katika banda la NSSF katika Maonyesho ya Biashara ya Kimataifa jijini Dar es salaam.
Mtanzania anayeishi nchini Marekani, Bernadeta Kaiza akiwashukuru Wajumbe wa Bodi ya wakurugenzi wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) baada NSSF kusafirisha mwili wa marehemu mume wake ambaye alikuwa mwanachama wa NSSF WESTADI, aliyefariki nchini Marekani hivi karibuni na Kuzikwa Tanzania ambapo NSSF iligharamia safari yote ya kuja Tanzania kwa ajili ya mazishi
Baadhi ya Wajumbe wa  Bodi ya wakurugenzi wa NSSF.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya jamii (NSSF) akizungumza na waandishi wa Habari. Katikati ni Mwenyekiti wa Bodi, Abubakar Rajabu.


DAR ES SALAAM Tanzania,

Mtanzania anayeishi nchini Marekani, Bernadeta Kaiza ametoa wito kwa watanzania wanaoishi ughaibuni  kujiunda na mafao ya Welfare Scheme  for Tanzanian Diaspora (NSSF WESTEDI) huduma ambayo itamuwezesha mwanachama kupata huduma ya kusafirishwa kutoka nchi husika mpaka nyumbani Tanzania pindi anapofariki.

Akizungumza katika banda la NSSF  mbele ya wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Taifa la hifadhi ya Jamii (NSSF) waliofanya ziara katika Maonyesho ya 36 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es salaam.

"Kujiunga NSSF WESTEDI kutasaidia mwanachama kugharamiwa safari ya kusafirisha mwili kutoka nchi yoyote mpka Tanzania na kuondokana hali ya kuchangihana fedha pindi mmoja wetu anapofariki."

Wakati mwingine tunashindwa kusafirisha mwili kutokana na kukosa fedha lakini kwa kupitia huduma hii ya NSSF WESTEDI sasa matatizo ya muda mrefu tuliyokuwa nayo sasa yatakwisha endepo watu wengi watajiunga na huduma hii kutokana na gharama zote za mwanachama kugharamiwa na NSSF, aliongeza Bi. Bernadeta Kaiza wakati akiishukuru Bodi ya Wakurugenzi wa NSSF kwa kufanikisha safari ya kuja Tanzania pamoja na mwili  wa marehemu mume wangu.

Akizungumza na Waandishi wa Habari, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la taifa la Hifandhi ya Jamii (NSSF), Dk Ramadhani Kitwana Dau amesema kuwa  ili kujiunga na mafao hayo mwanachama anatakiwa kutoa ada ya uanachama ambayo ni Dola za Marekani 300 kwa mwaka na fomu zinapatikana katika mtandao

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad