Mbunge wa Kigoma Mjini Mh. Peter Serukamba akipokea i-pad aina ya Samsung Galaxy kutoka kwa Meneja wateja wa mikataba wa Vodacom Tanzania Bi.Melinda Siara Kamukara Bungeni Mjini Dodoma. Mh. Serukamba ni miongoni mwa Wabunge wanaotumia na kufurahia huduma za mawasiliano za Vodacom chini ya utaratibu wa malipo ya baada.
Ofisa huduma za kiufundi kwa wateja wa mikataba wa Vodacom Bw. Dia Misana akiwaelekeza waheshimiwa Wabunge Raya Khamis (Viti Maalum - Chadema) na Francis Mkosamali (Kibondo - NCCR-Mageuzi) mwenye shati jeupe ambao ni wateja wa malipo ya baada wa Vodacom Tanzania namna ya kujiunga na kufaidi huduma bora za Intaneti za Blackberry (BIS) kupitia mtandao wa Vodacom katika viwanja vya Bunge mjini Dodoma.
Kutoka kulia Meneja wa Mahusiano ya nje wa Vodacom Tanzania Bw.Salum Mwalim, Melinda Siara Kamukara na Dia Misana wa kampuni ya Vodacom wakiwahudumia wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano ambao ni wateja wa mkataba wa Vodacom Tanzania.Zoezi hilo limefanyika Bungeni Mjini Dodoma ikiwa sehemu ya kujali wateja wake ambapo wabunge zaidi walijiunga na huduma hiyo.
No comments:
Post a Comment