Kampuni za valley spring na Mashujaa Investment Group zimejitokeza kudhamini shindano la kumsaka mrembo wa utalii wilaya ya kinandoni.
Akiongea na mwandishi wa habari hii jana jioni katika hoteli ya Travertine iliyopo magomeni jijini Dar es salaam. Mkurugezi wa miss utalii kinondoni Methuselah Magese alisema makampuni hayo yamejitokeza katika muda muafaka na ujio huo umezidi kuimarisha maandalizi ya shindano.
Jumla ya warembo 12 wanatarajiwa kupanda jukwaaani kuwania taji la miss utalii wilaya ya kinondoni ambapo shindano litafanyika katika hoteli ya travertine siku ya ijumaa ya tarehe 20 mwezi julai.
Magese alisema wanyange wanao wania taji hilo ni pamoja na Irene Richard, Lucia Joseph, Mwasiti Thabiti, Zahara Waziri, Janeth Nelson Winfrida Gration, Fatma Hussein na Neema Ngowi. Wengine ni Hellen Herman, Ruby Ramadhani, Arafa Mmanga, Doreen Pereus na Duda Harold.
Magese alisema miss utalii Kinondoni ni shindano lenye mvuto wa aina yake jijini Dar es salaam kwa kipindi hiki cha msimu wa majira ya baridi.

.jpg)
No comments:
Post a Comment