Sunday, July 15, 2012

TIMU YA MASHABIKI WA MACHESTER UNITED WACHUKUA KOMBE LA SERENGETI FIESTA SOCCER BONANZA



Ilao Ejakait Meneja wa Uendeshaji upande wa mauzo kampuni ya bia ya Serengeti akikabidhi zawadi kombe kapteni wa timu ya mashabiki wa klabu ya Manchester United ya Uingereza katika bonanza la Serengeti Fiesta Soccer Bonanza lililofanyika jana kwenye viwanja vya Sigara TCC Chang'ombe jijini Dar es salaam ,baada ya timu ya mashabiki hao kuwafunga mashabiki wa timu ya Bacelona na kuchukua kombe hilo Bonanza hilo lilishirikisha mashabiki wa vilabu mbalimbali vya Ulaya, katikati ni Allan Chonjo Meneja wa bia ya Serengeti Lager na kulia ni Bahati Singh Joseph Mahawi meneja Mauzo wa Serengeti.
Kapten wa timu ya mashabiki wa Manchester United akinyanyua juu juu kombe lao mara baada ya timu ya mashabiki hao kuwafunga mashabiki wa timu ya Bacelona na kuchukua kombe hilo kulia ni Ilao Ejakait Meneja Uendeshaji na mauzo kampuni ya bia ya Serengeti Allan Chonjo Meneja wa bia ya Serengeti Lager

Meneja mauzo wa kampuni ya bia ya Serengeti Joseph Mahawi (kulia) akikabidhi kombe la mshindi wa pili timu ya mashabiki wa Barcelona jana kwa kapten wa timu hiyo Michael Mashoto mara baada ya kuchukua nafasi ya pili katika bonanza la Serengeti Fiesta Soccer Bonanza kwenye viwanja vya TCC Chang;ombe kwa kufungwa na Manchester United

Mashabiki wa Manchester United wakishangilia baada ya kuingia fainali.

Wachezaji wa timu za mashabiki wa Manchester United na Barcelona wakichuana vikali katika mchezo wao wa fainali ambapo Manchester United ilishinda mchezo huo.

Mchuano mkali ukiendelea kwenye viwanja vya TCC Sigara.

Mashabiki wa timu ya Chealsea wakishangilia mara baada ya kuingia nusu fainali.

Wadau kutoka kampuni ya bia ya Serengeti nao walikuwepo kuhakikisha kila kitu kiko sawa kutoka kulia ni Kaisi, Bahati Singh Meneja Matukio na Promosheni Queen Sendiga Afisa wa Promosheni Kanda ya Dar es salaam na Ilao Ejakait Meneja wa Uendeshaji upande wa mauzo.
Mdau Heavy D. akiwa amekaa chini hoi huku jua likimpiga vibaya baada ya kukata tamaa kabisa kutokana na timu yake ya Arsenal kutolewa mapema katika bonanza hilo hapa anaonekana kama vile analalamikia kitu

Mashabiki wa Barcelona wakishangilia baada ya kuchukua ushindi wa pili katika bonanza hilo.

No comments:

Post a Comment