HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, July 6, 2012

Stive Nyerere akabidhi filamu yake mpya ya Mwalimu kwa mama Maria Nyerere

Mjane wa Baba wa Taifa,Mwalimu Julius Nyerere Mama Maria Nyerere akipeana mkono na Muigizaji wa filamu nchini kutoka Kundi la Bongo Movie,Steven Mangele "Stive Nyerere" pamoja na Wasanii wenzake alioongozana nao kwenda kumtembelea Mama Maria Nyerere nyumbani kwake Msasani jijini Dar.

Mwigizaji wa filamu nchini kutoka Kundi la Bongo Movie,Steven Mangele "Stive Nyerere" jana alikabidhi filamu yake aliyoiigiza kama Mwalimu Nyerere kwa Mama Maria Nyerere ikiwa ni kama shukrani zake, baada ya mama huyo kumsaidia katika kukamilisha filamu hiyo ambayo aliifanyia Butiama.

 Stive alisema kwamba kumpa filamu hiyo Mama Maria Nyerere ni kuweka kumbukumbu kwamba,anathamini msaada na mchango wake katika filamu hiyo na hana kikubwa cha kumpa wala cha kumfanyia zaidi. 

Amesema Mama Maria Nyerere alimsaidia sana katika kumuonyesha vitu gani mwalimu alikuwa akifanya, na vitu gani  mwalimu alikuwa akivipenda, na sehemu ambazo mwalimu alipenda kukaa baada ya kazi zake.

Pia ametoa shukrani kwa wasanii wenzake ambapo waliojitahidi katika hali moja au nyingine kuhakikisha filamu hiyo inakamilika.
Mama Maria Nyerere akisalimiana na Mwenyekiti wa Bongo Movie,Jacob Steven "JB".
Mama Maria Nyerere akiwa na Filamu alizokabidhiwa na Muigizaji,Steven Mangele "Stive Nyerere".
Mama Maria akitoa somo kwa Wasanii wa Bongo Movie waliomtembelea nyumbani kwake.
Picha ya pamoja.

1 comment:

  1. Steve you have done a realy great job. Hongera san Bongo Movies. Hizi ndio habari bana!!!

    ReplyDelete

Post Bottom Ad