HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, July 30, 2012

SERIKALI INAFANYA JITIHADA KUFIKISHA MAWASILIANO MAENEO YOTE NCHINI - MH. MAKAMBA

Na Veronica Kazimoto – MAELEZO,Dodoma

Serikali inaendelea kufanya utafiti kwa kumtumia mtaalam mwelekezi ambaye anatathimini mahitaji ya fedha na mbinu bora zenye gharama nafuu za kufikisha mawasiliano katika maeneo mbalimbali nchini.

Naibu Waziri wa Wizara ya Mawasilino, Sayansi na Teknolojia Mhe. Januari Makamba amesema Serikali inaendelea kufanya tathimini na mpaka sasa imekwisha hakiki mahitaji ya huduma za mawasiliano nchini na kubainisha zaidi ya vijiji 2175 ambavyo havina mawasiliano mazuri na kutokuwa na mawasiliano kabisa.

“Tathimini hiyo inatarajiwa kukamilika mwezi agosti 2012 ambapo zabuni mpya zinatarajiwa kutangazwa mwezi septemba 2012 kwa kuzingatia mapendekezo ya mtaalamu na kwa ajili ya hatua zaidi za utekelezaji,” ameongeza makamba.

Naibu Waziri huyo amesisitiza kuwa baada ya zoezi hilo kukamilika huduma za mawasiliano zitaboreshwa na kupatikana katika maeneo mbalimbali nchi nzima.

Zoezi hili lilianza mwezi novemba 2011 ambapo Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCAF) ulitekeleza awamu ya kwanza uliojumuisha vijiji 140 nchi nzima pamoja na uchambuzi na matokeo ya zabuni kwa ajili ya utekelezaji wa awamu hiyo ulikamilika mwezi machi mwaka huu.

Makamba ameyasema hayo wakati akijibu swali la mbunge wa jimbo la Solwa Ahmed Salum aliyetaka kujua ni lini serikali itapeleka mnara wa mawasiliano ya simu za mkononi katika kata ya Lyabukande kama ilivyoahidiwa na Mhe. Rais Jakaya Mrisho Kiwete.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad