Rais Jakaya Mrisho Kikwete akishiriki katika swala ya Magharibi na waumini wengine wa Mkoa wa Lindi aliowakaribisha katika futari Ikulu ndogo ya Mkoani Lindi Julai 30, 2012.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwashukuru waalikwa kwa kuhudhuria katika hafla ya futari aliyoandaa.
Kadhi wa Mkoa wa Lindi ambaye pia ni Shekhe Mkuu wa Mkoa Mohamed Saidi Mushangani akitoa neno la shukurani baada ya futari.
Mkuu wa Mkoa a Lindi Mhe Ludovick Mwananzila akishiriki katika futari hiyo pamoja na waalikwa wengine.
Waalikwa wakipakua futari.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na wageni waalikwa baada ya kufuturu.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Mkuu wa Magereza wa Mkoa wa Lindi (kushoto) na Mkuu wa Idara ya Uhamiaji ya mkoa waliokuwa miongoni mwa wageni waalikwa.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na wageni wake baada ya futari.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na wachungaji waliokuwa miongoni mwa wageni waalikwa.PICHA NA IKULU.











No comments:
Post a Comment