Mafundi na wataalamu wa Tanesco kanda ya Ilala wakimuonyesha mteja wao namna mita ya umeme ilivyochezewa ili iibe umeme wakati walipoendesha zoezi la ukaguzi wa mita kwenye eneo la Upanga jijini Dar es Salaam leo, kutokana na kitendo hicho mteja huyo alikatiwa umeme na kutakiwa kufika kwenye ofisi za kanda hiyo.
Wafanyakazi na wataalamu wa Tanesco wakiwa nje ya geti kwenye moja ya nyumba zilizokuwa zikikaguliwa mita za umeme baada ya wenyenyumba kukataa kufungua milango na badalayake kubandika kikaratasi kwenye geti kinachoonyesha namba za mita yao.
Meneja wa Tanesco kanda ya Temeke,Richard Mallamia akiwaonyesha waandsishi wa habari mita iliyochezewa na kuunganishwa umeme kinyume na mfumo wa kawaida ilikuiba umeme kwenye duka moja eneo la Kigamboni ambapo zoezi la kukamata wezi wa umeme linaendelea.
Mafundi wa Tanesco wakipitia pita iliyokuwa ikitumika kwa kuiba Umeme.
Wataalamu wa mifumo ya umeme na mafundi wa Tanesco kanda ya Temeke wakiangalia namna mita ilivyochezewa na kuiba umeme kwenye nyumba ya mfanyabishara Jamal Hassan eneo la Kigamboni na kuiba umeme.
Mfanyabishara duka na migahawa ya eneo la Kigamboni Jamal Hassan, akipanda kwenye gari la Tanesco kanda ya Temeke ili kumpeleka kwenye kituo cha polisi kutoa maelezo ya kwanini anaiba umeme.
Picha/Habari na Said Powa .
SHIRIKA la Umeme Tanesco kupitia kanda zake maalum za Ilala na Temeke leo limeendelea na operesheni zake za kukamata wezi wa umeme wanaochezea mita na wanaojiunganishia bila ya utaratibu maalum.
Wakizungumza kwenye operesheni hiyo kwanyakati tofauti Mameneja hao walieleza namna operesheni hizo zinavyosaiia kuwakamata wahalifi wa mita za umeme na kumekuwa na ufanisi mkubwa tangu kuanza kwa zoezi hilo.
Meneja wa kanda ya Ilala Mhandisi Athanasius Nangalia, mesema tangu zoezi hilo limeanza mwezi mmoja uliopita wamefanikiwa kukagua wateja 4700 na kufanikiwa kukamata wezi wa umeme 51 ambao kutokana na faini walizo lipa wamefanikiwa kukusanya shilingi 45 Millioni.
Aidha Nangali alifafanua kua pamoja na ukusdanyaji huo pia waligundua watu wanaojiunganishia umeme bila ya utaratibu kwa kujiwekea nguzo zao wenyewe lakini wamedhibiti vitendo hivyo kwa kukamata nguzo 18 kwenye maeneo mbalimbali ya Ilala.
Aidha kwenye zoezi lililoendelea leo eneo la Upanga liliambatana na vituko kutoka kwa wenye nyumba baada ya kujifungia ndani na kukataa wakaguzi hao wasiingie ndani ya nyumba hizo hata hivyo waliamua kubandika ujumbe kwenye mageti hayo unaoeleza namba za mwisho za mita zilizo somwa na zilizopo sasa.
KWA UANDE WA Temeke zoezi hilo limefanyika eneo la kigamboni na kufanikisha kutiwa mbaroni kwa watu watatu ambao wanatuhumiwa kujihusisha na wizi wa umeme.
Mhanyabiashara mmoja Jamal Hassan alikutwa akiwa na mita mbili ambazo pamoja na kutumia umeme lakini mita hizo hazisomi na wala umeme hauishi hatakama akiwasha vifaa vyake vyote hali iliyowalazimu wakaguzi hao kukata umeme na kumshikilia kwa mahojiano zaidi.
Akifafanua zaidi Meneja wa kanda ya Temeke Richard Mallamia, amesema vitendo hivyo vimekua vikiendelea lakini mwishowake ndio huu kwani kutokana na mifumo inayotumika kwa sasa wanamtambua moja kwamoja mwizi wa umeme hata bila yakwenda nyumbani kwa mteja kutokana na kufunga vifaa vinavyofuatilia matumizi ya umeme kwa mteja.
“Hili zoezi haliwi gumu sana kwakua tunakwenda sehemu ambazo tuna hakika kuna watu waniba umeme na kweli tukifika tunawakamata,” Alisema Mallamia.
Mpaka sasa watu 13 wanatarajiwa kufikishwa mahakamani muda wowote baada ya kukamilika taratibu za mashitaka kutokana na wizi huo.
Kiasi cha Pesa kilichokusanywa kutokana na faini na madeni kwenye kanda hiyo kimefikia Tsh40 kati ya kiwango cha umeme kinachopotea kwa mwezi cha Tsh89Millioni.
No comments:
Post a Comment