Ajari hii imetokea leo katika barabara ya Nyerere Road/Pugu Road maeneo ya AfriCare karibu na kiwanda cha Pepsi jijini Dar ambapo gari hii aina ya Jiafeng iliyokuwa imebeba maji masafi ilikuwa ikijaribu kukata kona kuingia kulia bila kuangalia gari zilizokuwa zikitoka moja kwa moja airport na kujikuta ikipigwa kwenye bodi na gari nyingine aina ya Toyota Land Cruser iliyopelekea kunyofoka kwa bodi ya lori hilo...hakuna aliyepoteza maisha.
Gari iliyokuwa ikitokea njia ya airport ikiwa haitamaniki kwa mbele baada ya kuigonga lori hilo.
Kila aliekuwa akipita eneo hilo alibaki kushangaa na kutoamini kilichotokea.
Wazee wa Break Down a.k.a wa Mizoga wakiifunga gari hii ili kuipeleka mahali husika.






No comments:
Post a Comment