HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, July 16, 2012

Mtaa unapogeuzwa Dampo la Takataka jijini Mbeya

Mtaa wa mwambenja uliopo maeneo ya uzunguni  jijini Mbeya umeanza kufutika katika ramani ya jiji la mbeya baada ya mtaa huo kugeuzwa dambo la takataka na si barabara tena ya kupita magari na wakazi wa eneo hilo la uzunguni kama ilivyokuwa hapo awali.
Kibao kinachoonyesha mtaa wa Mwambenja kulia ndiyo mtaa ambao barabara yake imefutika kutokana na takataka na vichuguu vya nyasi vilivyopo mtaani hapo kana kwamba hakukuwa na Mtaa wowote.

Hii ndiyo barabara ya mtaa huo wa Mwambenja uzunguni jijini Mbeya,ambapo zamani ilikuwa yanapita magari lakini siku hizi hata Bajaj haipiti.
Hizi ni takataka zinazotupwa mtaani hapo
Kwa ujumla kipande cha mtaa wa Mwambeja sasa hakina barabara ya uhakika
kwa mbele huku mambo ndio yako namna hii.Picha na Mbeya Yetu Blog

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad