HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, July 24, 2012

mchezo wa yanga na Mafunzo uwanja wa Taifa jijini Dar leo,Mchezaji wa Mafunzo,Juma Mmanga apoteza fahamu uwanjani

 "Hupiti hapa" hivyo ndivyo alivyokuwa akimaanisha Kiungo wa Timu ya Mafunzo ya Zanzibar,Mohamed Abdulrahim wakati akimzuia Mpinzani wake wa Timu ya Yanga,Juma Abdul wakati wa mchezo wao wa hatua ya Robo Fainali ya Mashindano ya Cecafa Kagame Cup,katika uwanja wa Taifa jijini Dar leo.Yanga imeshinda kwa mikwaju ya penati 5-4.
 Mshambuliaji wa Yanga,Hamis Kiiza akitaka kumtoka Beki wa Mafunzo.
 Nyanda wa Timu ya Mafunzo akiokoa Moja ya Hatari zilizokuwa zikielekezwa langoni kwake.
 Mikwaju ya Penati ikipigwa.

SEKESEKA LA KUPOTEZA FAHAMU MCHEZAJI WA MAFUNZO: Ilikuwa ni mpira wa krosi iliyopigwa na Mchezaji wa Yanga,Juma Abdul kuelekea langoni mwa timu ya Mafunzo na ndipo Mchezaji wa Timu ya hiyo ya Mafunzo kutoka Zanzibar,Juma Mmanga (13) aliruka juu Sambamba na Mshambuliaji wa Timu ya Yanga,Hamis Kiiza na kugongana kwa bahati mbaya wakiwa katika harakati hiyo ya kuwania mpira wa juu,hali iliyopelekea Mchezaji huyo wa Mafunzo ya Zanzibar,Juma Mmanga kupoteza fahamu na kufanya mchezo huo kusimama kwa muda.Mchezo huo uliendelea baadae na kumalizika kwa hatua ya Penati ambao timu ya Yanga iliweza kuibuka mshindi baada ya kushinda mabao 5-4.
 Wachezaji wa Timu zote mbili za Mafunzo na Yanga wakisaidiana kumpepea Mchezaji Juma Mmanga wa Mafinzo baada ya kupoteza Fahamu kutoka na kugongana kwa bahati mbaya na mchezaji mwenzie wa Yanga,Hamis Kiiza.
 Wachezaji wa Timu ya Mafunzo wakiwa wamechanganyikiwa baada ya mwenzao kupoteza fahamu wakati wa mchezo wa Mashindano ya Kombe la Cecafa Kagame dhidi ya Timu ya Yanga uliochezwa jioni ya leo kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar.
 Wafanyakazi wa Chama cha Msalaba Mwekundu wakimtoa mchezaji huyo uwanjani chini ya Uangalizi wa Madaktari wa Timu zote mbili kwa ajili ya kumpatia huduma ya kwanza.
 Wafanyakazi wa Chama cha Msalaba Mwekundu wakimpeleka katika chumba ya huduma ya kwanza Mchezaji wa timu ya Mafunzo,Juma Mmanga baada ya kupoteza fahamu.
 Baadae alizinduka lakini hali yake haikuwa nzuri hivyo,ililazimika mchezaji huyo apelekwe hospitali kwa matibabu zaidi.
Mchezaji Juma Mmanga akiagana na Mmoja wa wachezaji wenzake aliekuwa nae wakati akiingizwa kwenye gari la Wagonjwa Mahututi tayari kwa safari ya hospitalini.
Penati ya mwisho ya timu ya Yanga iliyopigwa na Athuman Iddy ndiyo iliyowatoa Mafunzo katika Mashindano ya Cecafa Kagame Cup jioni ya leo kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad