HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, July 4, 2012

Maonyesho ya Sabasaba katika picha

Meneja uhusiano Mwandamizi wa Benki ya Posta Noves Moses (kulia) akitoa ufafanuzi kwa wananchi juu ya huduma za Benki hiyo popote(TPB Popote) ambapo mteja anaweza kutoa na kuweka pesa zake popote alipo . Meneja huyo alitoa maelezo hayo jana jijini Dar es salaam kwenye banda la Wizara ya Fedha wakati wa maonesho ya 36 ya biashara ya kimataifa ya Dar es salaam yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu J.K.Nyerere. (Picha na MAELEZO-Dar es salaam).
 Waziri mkuu wa Serikali ya Wanafunzi wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha(IFM) Sarungi Daniel (kulia) akimwelekeza mwananchi juu ya taratibu ya kujiunga cha IMF katika kozi mbalimbali jana jijini Dar es salaam wakati mwananchi huyo alipotembelea banda la Wizara ya Fedha katika Maonyesho ya 36 ya kimataifa ya Dar es salaam yanayoendelea.
 Afisa Mafao wa Mfuko wa Akiba wa wafanyakazi serikalini (GEPF) Deogratius Urio (kulia) akisikiliza maswali mbalimbali  kutoka kwa Askari Polisi jana jijini Dar es salaam waliotaka kujua faida za kujiunga na Mfuko wakati walipotembelea banda la Wizara ya Fedha  kwenye  maonesho ya 36 ya biashara ya kimataifa ya Dar es salaam yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu J.K.Nyerere.
Afisa Manunuzi kutoka Dhamana ya Uwekezaji Tanzania(UTT) Hamis Kiimbi (kulia) akimwelekeza mwananchi juu ya taratibu ya kuwekeza katika mfuko huu jana jijini Dar es salaam wakati mwananchi huyo alipotembelea banda la Wizara ya Fedha katika Maonyesho ya 36 ya kimataifa ya Dar es salaam yanayoendelea.
 Afisa Habari na Mawasiliano wa Mfuko wa Changamoto za Melenia Tanzania (MCAT) Josephat Kinyunyu (kushoto) akitoa maelezo kwa wananchi jana jijini Dar es salaam kuhusu miradi mbalimbali inayosimamiwa na mfuko huo wakati wananchi hao walipotembelea banda la Wizara ya Fedha  kwenye  maonesho ya 36 ya biashara ya kimataifa ya Dar es salaam yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu J.K. Nyerere.Picha na Habari Mseto Blog.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad