SHINDANO maalum lililotamba miaka ya nyuma la Maisha Plus,ambalo washiriki wake hukaa kwa miezi miwili kijijini, linatarajiwa kuanza hivi karibuni kwa kushirikiana na shirika la Oxfam Tanzania, kupitia program yake ya‘Mama shujaa wa chakula’.
Akizungumza kwa jana, Kiongozi Mtendaji wa kampuni ya DMB,Masoud Ali ‘Masoud Kipanya’ alisema kuwa, shindano hilo la aina yake linakujatena kwa msimu wa tatu, likiwa na utofauti kabisa, huku mambo mbalimbaliyakiboreshwa, ikiwemo mshindi kuibuka na kitita cha sh milioni 20.
Kipanya alisema kuwa, kwa kushirikiana na wadhamini wakuu,Oxfam Tanzania, kupitia program yao ya ‘Mama shujaa wa chakula’, ambakowatapata fursa ya kuwaweka wanawake kwenye shindano, kwa kukaa ndani ya jumbahilo la Maisha Plus huko kijijini kwa wiki mbili.
“Kwa kushirikiana na Oxfam, shindano hili tumeborsha nalitakuwa la aina yake, ambapo washiriki watakaobahatika kushiriki, watafurahiana watajifunza mengi na safari hii Mama shujaa wa chakula nao watabahatikakukaa kwa wiki mbili, kisha watatoka na washiriki wa Maisha Plus kuendelea nakinyang’anyiro cha kuwania kitita hicho cha milioni 20,” alisema Kipanya.
Aidha, aliwataka vijana wa kitanzania, kuchangamkia fursahiyo, ambako wanatarajia kuanza kufanya usaili mkoani Arusha, Agosti 3 na kishakuendelea kwenye mikoa mingine 14, ikiwemo ya Bara na viswani Zanzibar.
Pia, alitoa wito kwa wadhamini wengine, kutumia nafasi hiikujitokeza ili kupata kutangaza, kwani shindano hilo licha ya kufanyika misimumiwili ya 2009 na 2010, huku 2011likishindwa kufanyika kutokana na kukosa udhamini, limejizolea sifa na kupendwana watu wa rika mbalimbali.


No comments:
Post a Comment