Bendi ya African Stars “Twanga Pepeta” kuanzia tarehe 1 July 2012 itakuwa ikitoa burudani katika ukumbi wa Mzalendo Pub uliopo maeneo ya Makumbusho katika jengo la Millenium Tower.
Burudani itakuwa ikitolewa ukumbini hapo kwa kila siku za Jumapili mara baada ya kumalizika kwa Bonanza linalofanyika kila siku za Jumapili mchana kuanzia saa nane mpaka saa mbili za Usiku.
Twanga Pepeta wameamua kutoa burudani ukumbini hapo mara baada ya kuitikia maombi ya muda mrefu kutoka kwa wapenzi wa Twanga Pepeta wanaoishi maeneo ya jirani na Mzalendo Pub.
No comments:
Post a Comment