HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, June 10, 2012

Taifa Stars yaichabanga bao 2-1 timu ya Gambia jijini Dar leo

Kikosi kilichofanya mauaji leo
Kaseja akiokoa moja ya hatari langoni Stars

Taifa Stars jioni hii imeibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Gambia kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, katika mechi ya pili ya Kundi C, kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Kombe la Dunia mwaka 2014 nchini Brazil.

Stars ilitoka nyuma kwa 1-0 kipindi cha kwanza na kuibuka na ushindi huo- kwa mabao ya kipindi cha pili ya Shomari Kapombe dakika ya 60 na Erasto Nyoni dakika ya 87 kwa penalti, baada ya beki mmoja wa Gambia kuunawa mpira kwenye eneo la hatari.

Stars ambayo mechi ya kwanza ilifungwa 2-0 na wenyeji Ivory Coast mjini Abidjan Jumamosi iliyopita, kipindi cha kwanza ilicheza ovyo kidogo, lakini kuingia kwa Haruna Moshi ‘Boban’ aliyechukua nafasi John Bocco ‘Adebayor’ kipindi cha pili, kuliifanya Tanzania icheze kwa uhai na kulitia misukosuko lango la Gambia hatimaye kupata mabao hayo mawili.

Gambia walitangulia kupata bao lililofungwa na Mamadou Ceesay dakika ya nne. Stars sasa imejinasua mkiani mwa kundi C na kupanda nafasi ya pili badaaye Morocco kutoa sare ya 2-2 jana na Ivory Coast inayoongoza kwa pointi zake nne.

Kwa Stars huu ni ushindi wa kwanza nyumbani tangu waifunge Jamhuri ya Afrika ya Kati Machi 26, mwaka jana.
Picha na Habari na  Bin Zubeiry

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad