HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, June 26, 2012

MASHINDANO YA NGOMA ZA ASILI YA BALIMI EXTRA LAGER 2012 KUTIMUA VUMBI KUANZIA JUNI 30

Meneja Meneja Masoko wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Fimbo Butallah akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya uzinduzi wa mashindano ya ngoma za asili ya balimi yanayotarajiwa kuanza kwenye mikoa ya kanda ya ziwa june 30.Kushoto ni Meneja wa Bia ya Balimi Edith Bebwa
Meneja wa bia ya Balimi Edith Bebwa akizungumza na waandishi wa habari juu ya uzinduzi wa mashindano ya ngoma za asili ya balimi yanayotarajiwa kuanza kwenye mikoa ya kanda ya ziwa june 30 kulia ni Meneja Meneja Masoko wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Fimbo Butallah.

Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), kupitia bia yake ya Balimi Extra Lager, leo imezindua rasmi mashindano ya ngoma za asili ya Balimi Extra Lager kwa mwaka 2012. Mashindano haya ambayo yametokea kupendwa sana na wakazi wa kanda ya ziwa yanatarajiwa kuanza kutimua vumbi katika mikoa mbali mbali ya kanda ya ziwa kuanzia Juni 30.

Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi huo Jijini Dar es Salaam, meneja wa Bia ya Balimi Extra Lager Bi. Edith Bebwa alisema; Bia ya Balimi Extra Lager imekuwa ikiendesha mashindano haya maarufu kama “Mashindano ya Ngoma za Asili ya Balimi Extra Lager” kwa zaidi ya miaka saba sasa , na kwa kweli napenda kusema kuwa ni mashindano yaliyotokea kupendwa sana katika kanda yetu hii ya ziwa,Lengo kuu la kudhamini mashindano haya ni kushirikiana na wakazi wa kanda ya ziwa katika kuenzi na  kulinda tamaduni za kanda alisema Bi Edith .
Kwa mwaka huu wa 2012, mashindano yataanza rasmi tarehe 30 Juni katika ngazi za mikoa na kumalizika tarehe 21 Julai. Tutaanza na mkoa wa Mwanza ukifuatiwa na mikoa ya Mara, Kagera, Shinyanga na Tabora, katika mpangilio ufuatao.

Tarehe
Mkoa
Viwanja
30/06/2012
KAGERA

Kaitaba
07/07/2012
MWANZA
Ccm Kirumba
14/07/2012

TABORA
Chipukizi
21/07/2012

SHINYANGA
Shycom
21/07/2012

MUSOMA
Bwalo la Magereza
28/07/2012.

FINALS MWANZA
Ccm Kirumba

Akielezea juu ya zawadi za mwaka huu, bi. Edith Bebwa alisema; kama ilivyo ada ya Bia ya Balimi, kila mwaka tumekuwa tukiongeza zawadi ili kuongeza chachu ya ushindani na kuleta tija kwa washindani. Kwa mwaka huu tumeongeza zawadi kwa takribani asilimia 20 ukilinganisha na mwaka jana. Hii yote inaonesha jinsi gani bia ya Balimi inatambua, inajali na kuthamini utamaduni wa kanda yetu. Zawadi kwa washindi ni kama ifuatavyo;


Ngazi ya mkoa
Finali
 Mshindi wa kwanza
          600,000
                  1,100,000
 Mshindi wa pili
          500,000
                     850,000
 Mshindi wa tatu
          400,000
                     600,000
 Mshindi wa nne
          300,000
                     500,000
 Mshindi wa tano hadi wa kumi kila kikundi
150,000
250,000

Pamoja na zawadi hizi nono, pia Balimi Extra Lager itaendelea kutoa huduma muhimu kwa vikundi shiriki kama vile chakula na malazi. Tunaamini kabisa mambo yote haya yataongeza hamasa na msisimko katika mshindano ya mwaka huu. Na kauli mbiu yetu kwa mwaka 2012 Balimi Extra Lager, twajivunia utamaduni wetu.

Akizungumzia maandalizi ya fainali hizo, Meneja Masoko wa Tbl Fimbo Buttalah alisema; Maandalizi yote kwa upande wetu sisi wadhamini yameshakamilika, hivyo niwaombe tu washiriki wote ambao nimepata taarifa kuwa wamekuwa mazoezini kwa muda sasa, waendelee na mazoezi ili kuonesha uwezo wa juu utakaoleta ushindani na kutoa burudani yenye kiwango cha juu.

Kwa niaba ya bia ya Balimi Extra Lager, tunapenda kuwakaribisha watu wote kuhudhuria mashindano haya ambayo tarehe na mahali yatakapofanyikia zitakuwa zikitangazwa redioni ili waweze kushuhudia burudani hii na kuuenzi utamaduni wetu. 

Pia wananchi wasisahau kuwa katika burudani hizi pia wataburudika na Bia yao waipendayo ya Balimi Extra lager baridi, na kushinda zawadi mbali mbali katika promosheni za Balimi zitakazoambatana na Mashindano haya ya Ngoma za asili ya Balimi Extra Lager.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad