HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, June 30, 2012

MABONDIA WA BIGRIGHT YA MWANANYAMALA WAAHIDIWA BAISKELI

 Hawa ni mabondia wa Bigright Boxing Club walioteuliwa kuanza kazi. Toka kushoto ni ISSA OMAR, MARTIN RICHARD,kocha Ibrahim,MWAITE JUMA na HERMAN SHEKIVULI ambao wote watacheza Julai 15, 2012.

Mabondia wa klabu ya mazoezi ya bigright ya mwananyamala wameahidiwa baiskel na katibu kata wa vijana wa CCM kinondoni REHEMA MBEGU ili ziwasaidie kwenda mashuleni mwao na mazoezini,Rehema mbegu mara nyingi huwa yupo karibu sana na vijana hao katika ushauri na kuwasaidia chakula na vinywaji wakati wakijiandaa na mashindano mbalimbali ,safari hii ameamua kutoa baiskeli ili kuhamasisha ushindani zaidi na kuwapa moyo vijana kupenda zaidi michezo kuliko vijiwe.


Baada ya kuhakikishiwa kuwa kila bondia atakae shinda toka klabu ya ngumi ya bigright atazawadiwa baskeli,wameahidi kukatika mikono ulingoni yaani ni lazima washinde na wamebadilisha mfumo mzima wa
mazoezi,kwa sasa wapo pamoja,kikambi zaidi nyumbani kwa kocha wao Ibrahim bigright na kuongeza muda zaidi wa mazoezi kwa sasa wanafanya mara tatu hadi nne kwa siku.



Mabondia hao ambao wanategemea kupanda ulingoni july 15 DDC-kariakoo ni Issa Omar(bigright boxing) atakaechapana na Ramadhan Kumbele toka kambi ya matumla katika uzani wa fly,Mwaite juma toka bigright boxing atapigana na mkongwe Anthony Mathias katika uzani wa bantam.



Ambao watakuwa wakisindikiza pambano la ubingwa wa taifa kati ya JUMA FUNDI wa keko na BAINA MAZOLA wa mabibo toka kambi ya mzazi.,  Mapambano hayo yameandaliwa na kaike siraju na kusimamiwa na TPBO

 Mabondia wa Bigright boxing Club wakiwa mazoezini

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad