HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, June 16, 2012

maadhimisho ya siku ya Mtoto wa Afrika jijini Mwanza leo

Maandamano ya watoto kuelekea uwanja wa michezo wa Nyamagana yaliyofanyika asubuhi hii jijini Mwanza.Siku ya Mtoto wa Afrika huadhimishwa tarehe 16, Juni ya kila mwaka. Siku hii inaadhimishwa kwa Azimio la nchi 51 wanachama wa uliokuwa Umoja wa Nchi huru za Afrika (OAU) kwa ajili ya kukumbuka mauaji ya kinyama waliofanyiwa watoto wa kitongoji cha Soweto nchini Afrika ya Kusini mnamo mwaka 1976.Siku hii huadhimishwa kwa lengo la kukumbuka mauaji ya kinyama waliofanyiwa watoto nchini Afrika ya Kusini wakati wakidai haki zao za msingi, pia kuwakumbusha wazazi/walezi na jamii kwa ujumla juu ya haki na wajibu wa jamii katika kuwalea watoto. Aidha, hutoa nafasi ya kuwakumbusha watoto haki na wajibu wao kama watoto katika Taifa.Picha na G Sengo Blog.

1 comment:

  1. Kuna haja ya serikali kuweke sheria kali yenye meno ambayo idhiti manyanyaso dhidi ya watoto hasa wenye ulemavu kwani kuna baadhi ya wazazi wanawafungia ndani watoto wenye ulemavu na kuwakozesha elimu

    ReplyDelete

Post Bottom Ad