HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, June 30, 2012

JIJI LA ARUSHA LATISHA KWA UCHAFU

Hili ni godoro kwa mtu huyu ambaye hakujulikana jina lake akiwa amelala katikati ya rundo la taka katika jalala la soko kuu la jijini Arusha kama alivyokutwa na kamera yetu wachuuzi katika soko hilo na wananchi wapitao pembeni ya jalala hilo wameilalamikia kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa kwa kufumbia macho vitendo vya uhalifu vinavyofanywa na vijana wakao na kupekua taka kwenye dampo hilo kila uchwao na kutochukukiwa hatua yeyote.






Mama huyu sawa katandika mfuko kisha akatandaza mchicha wake lakini majimaji aliyonyunyiza kwenye bidhaa yake yamepenya hadi chini kuungana na ardhi ambayo si salama kwa uwekaji chakula hali inayohatarisha afya ya mlaji. Malalamiko ya jiji hilo kuendelea kuwa chafu yamekuwa yakipuuziwa na viongozi wa halmashauri hiyo kwa visingizio vya kuwa bize na ripoti ya mkaguzi wa serekali CAG na kulitelekeza jiji katika hali hii

sehemu ya machinga wakiwa wamepanga bidhaa zao mbele ya maduka kama iliovyokuwa mtaa wa kongo jijini Dar na halmashauri kulifumbia macho kwa visingizio vya kuwaogopa na kushindwa kutekeleza sheria hali inayofanya msongamano katika barabara kadhaa za jiji hili na mbaraza ya maduka wafanyabiashara ya maduka wameilalamikia halmashauri hiyo kwa kukaa kimya bila ya majibu yakinifu.


Biashara mbele ya biashara ndani ya jiji la Arusha.

Mifereji aibu tupu hakuna usafi unaofanyika.
Mama ntilie wakiwa wamepanga vyakula vyao sehemu hatarishi bila ya kuogopa magonjwa, wala afya za walaji na halmashauri ikiwa inaona hali hiyo na kuilea kwa kusema kuwa eti ni sehemu ya kipato kwani mama ntilie hao wamekuwa wakiilipa halmashauri hiyo fedha za kuuzia eneo hilo zinazochukuliwa na kampuni inayokusanya fedha za ushuru wa geti na magari yanayoingia na kutoka katika stand kuu.
Uchafu umekidhiri kwa katika jiji hili 'nililo zaliwa mie' kiasi kwamba hata hadhi ya jiji la Utalii naona kama inapotezwa hivi labda tuite ...., hata hivyo ni aibu, au watendaji kazi wa halmashauri wanajivunia na hali hii, mabwana na mabibi afya mpo au ni sifaaaa? Kwa mpango huu naona ipo haja ya  kuanzishwa kwa tuzo ya jiji linaloongoza kwa uchafu nchini Tanzania.Naomba kuwasilisha... Picha zote na Libeneke la Dada Woinde Shizza wa Arusha.

2 comments:

  1. ARUSHA NI MJI MCHAFU MIE SIJAWAIKUONA, ETI NI JENEVA YA TZ. WANASHINDWA HATA KUIGA MFANO WA JIRANI ZAO MOSHI. MVUA IKANYESHA KIDOGO HUTAPATAMANI PANAVONUKA. MANISPAA MPO!!!? AU UFISADINKILA KONA

    ReplyDelete
  2. Arusha mnatia aibu! haiwezekani hela zote zinazoingia kwa njia ya utalii na vyanzo vingine vingi vishindwe kusafisha jiji, kazi kujaza matumbo yenu tu wakubwa hapo juu, acheni tamaa na mfanye kazi zenu ipasavyo...

    ReplyDelete

Post Bottom Ad