Majaji wa Epiq Bongo Star Search 2012, Master J, Salama Jabiri na Madam Ritha wakimsikiliza mmoja wa washiriki kwa umakini.
Mwanadada huyu akiimba kwa hisia kali wimbo wa Alicia Keys wa Sometime.
Mmoja wa washiriki wa Epiq Bongo Star Search 2012 akiimba mbele ya majaji.
Mkuu wa mawasiliano wa kampuni ya simu ya mkononi wa Zantel Awaichi Mawala (kushoto) akijumuika kuimba na washiriki waliojitokeza katika usaili huo.
Idadi kubwa ya vijana waliojitokeza katika usaili huo wakiwa wamekusanyika sehemu moja na kuimba pamoja.
Na Mwandishi Wetu
UWANJA wa burudani uliopo katika eneo la Ngome Kongwe leo ulifurika maelfu ya vijana waliojitokeza kushiriki katika kinyang’anyiro cha kuchaguliwa kuingia katika fainali za shindano la Epiq Bongo Star Search 2012.
Huku kukiwa na idadi kubwa ya washiriki wasichana pia kulikuwa na washiriki ambao waliwasili wakiwa na vifaa mbalimbali vya kupigia muziki kama vile gitaa,vinanda na vinginevyo ikiwa ni mikakati yao ya kujihakikishia kuchaguliwa.
Akizungumzia usaili wa Zanzibar Jaji Mkuu wa EBSS 2012 Ritha Paulsen alisema kuwa ameguswa na mwamko wa washiriki kutoka Zanzibar.
‘Zanzibar ina vijana wengi wenye vipaji na ambao wanatakiwa kuendelezwa ili kufikia malengo yao katika muziki’ aliongeza Ritha.
Alisema kuwa kupitia shindano la EBSS ambalo linadhaminiwa na kampuni ya simu za mkononi Zantel anatarajia kupata vipaji vingi katika mikoa yote ambayo usaili unaendelea.
Naye Mkurugenzi wa Biashara wa Zantel kwa Zanzibar Mohamed Mussa mbali na kufurahishwa na idadi kubwa ya washiriki waliojitokeza aliwataka vijana wa kisiwani hapa kutambua kuwa muziki unaweza kuwapatia ajira kubwa.
‘Muziki ni ajira, na ndio maana sisi Zantel tumeamua kuwekeza kwenye mashindano haya ili kuwapa fursa vijana wengi zaidi’ alisisitiza bwana Mussa.






No comments:
Post a Comment