HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, May 21, 2012

Uzinduzi wa Ndege Mpya ya Air Tanzania katika picha

 Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la ndege la Tanzania (ATCL), Bw. Paul Chizii akikata utepe kuashiria uzinduzi wa ndege mpya ya shirika hilo aina ya Boeing 737-500 kwenye uwanja wa ndege wa Mwanza iliyozinduliwa mwishoni mwa wiki iliyopita na kuanza safari zake rasmi katika mikoa ya Kilimanjaro- Mwanza na Dar es salaam wanaoshuhudia uzinduzi huo ni wafanyakzi wa ndege hiyo kulia Erica na kushoto Doris.
 Ndege hiyo ikiwa imetua kwenye uwanja wa ndege wa Kilimanjaro (KIA)
 Keki ikiingizwa kwenye ndege na mfanyakazi wa ndege hiyo Erica kwa ajili ya uzinduzi rasmi wa ndege hiyo.
 Abiria pamoja na baadhi ya wafanyakazi wakiwa ndani ya ndege hiyo.
Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la ndege la ATCL, Bw. Paul Chizii akisalimiana na abiria mbalimbali waliokuwemo katika safari za kuzindua ndege hiyo.
 Wafanyakazi wa shirika hilo pamoja na wale wa Kilimanjaro International Airport wakipunga mikono yao kuikaribisha ndege hiyo wakati ilipowasili katika uwanja huo.
 Baadhi ya Abiria wakishuka kwenye ndege kwenye uwanja wa ndege wa (KIA)
 Baadhi ya Abiria wakishuka kwenye uwanja wa ndege wa Mwanza.Picha na Full Shangwe Blog.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad