Mgeni rasmi kwenye ufunguzi wa warsha ya Mpango wa Msaada wa Kisheria Barani Afrika iliyoandaliwa na UNDP,Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mh. Angela Kairuki akisoma hotuba wakati akifungua rasmi warsha ya Mpango wa Msaada wa Kisheria Barani Afrika iliyoandaliwa na UNDP na kuhudhuriwa na wadau wa masuala ya sheria kutoka mataifa mbalimbali barani Afrika wakiwemo wenyeji Tanzania.
Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa Tanzania, Dk. Alberic Kacou akizungumza wakati wa ufunguzi wa warsha ya Mpango wa Msaada wa Kisheria Barani Afrika iliyoandaliwa na UNDP.Dk. Kacou amesema warsha hii ya Msaada wa Kisheria ni hatua nyingine katika kuelekea kuondoa vikwazo katika uwezeshaji wa Kisheria na kupatikana kwa haki kitu ambacho kimeathiri kwa kiwango kikubwa bara hili katika nyanja mbalimbali ikiwa ni pamoja na maisha ya watu, mali, Uraia, huduma za kijamii na kukosekana kwa fursa za maendeleo. Kulia ni Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mh. Angela Kairuki na kushoto ni mmoja wa maafisa wa makao makuu ya UNDP New York Shelley Inglis.
Baadhi ya wadau wa masuala ya sheria kutoka mataifa mbalimbali barani Afrika wakiwemo wenyeji Tanzania wakisikiliza hotuba ya mgeni rasmi Mh. Angela Kairuki.

No comments:
Post a Comment