HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, May 30, 2012

RAIS KIKWETE AFANYA MAZUNGUMZO NA RAIS WA IVORY COAST JIJINI ARUSHA

Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Rais  Allasane Ouattara  wa Ivory Coast wakiwa katika mazungumzo rasmi katika hoteli ya Ngurdoto jijini Arusha leo May 30, 2012 ambako Rais huyo wa Ivory Coast amefika kuhudhuria mkutano wa afDB ambao unbafunguliwa rasmi kesho na Rais Kikwete katika ukumbi wa AICC. Katika maongezi yao Rais Kikwete amesema Tanzania inaunga mkono juhudi za Ivory Coast za kutaka kurejesha nchini humo makao makuu ya afDB ambayo yamehamia Tunisia kutokana na vurugu zilizotokea Abidjan baada ya uchaguzi mkuu mwaka jana.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Rais  Allasane Ouattara  wa Ivory Coast wakiangalia shamba la kahawa wakati wakielekea  kwenye sehemu waliyotengewa kufanyia mazungumzo rasmi katika hoteli ya Ngurdoto jijini Arusha leo May 30, 2012 ambako Rais huyo wa Ivory Coast amefika kuhudhuria mkutano wa afDB ambao unbafunguliwa rasmi kesho na Rais Kikwete katika ukumbi wa AICC. Katika maongezi yao Rais Kikwete amesema Tanzania inaunga mkono juhudi za Ivory Coast za kutaka kurejesha nchini humo makao makuu ya afDB ambayo yamehamia Tunisia kutokana na vurugu zilizotokea Abidjan baada ya uchaguzi mkuu mwaka jana.
PICHA NA IKULU

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad