HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, May 22, 2012

msondo ngoma kusindikiza uzinduzi wa ukumbi mpya Emirate wilayani Masasi

Na Mwandishi Wetu

BENDI Kongwe ya Muziki wa Dansi,Msondo ngoma ya jijini Dar es salaam inatalajia kufanya uzinduzi wa ukumbi mpya kabisa na wa kisasa wa burudani wa Emirate Hall uliopo Masasi,mkoani Mtwara June 2 mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa habari Msemaji wa bendi hiyo Rajabu Mhamila 'Super D' Alisema wamealikwa kwa ajili ya kutoa burudani siku ya ufunguzi wa ukumbi huo ambapo watatoa burudani isiyo na kifani

"unajua sisi ni baba ya Muziki nchini ndio maana wapenzi wengi wanahitaji burudani kutoka kwetu ndio mana tunapopata nafasi ya kwenda mikoani tunakwenda kama hivi tumealikwa kutoa burudani siku hiyo tutatoa burudani ya uhakika".

Aliendelea kusema kuwa siku hiyo Msondo watapiga vibao vya vyote vya zamani na vipya ambavyo baadhi yake ni  Suluhu wa Shabani Dede, Nadhiri ya Mapenzi wa Juma Katundu na Baba Kibene wa
Eddo Sanga hizo ni baadhi ya nyimbo mpya zitakazonogesha siku hiyo vile vile watapiga nyimbo zao za zamani zilizotamba wakati huo Alisema Super D.

Kundi hilo litaambatana na wanamziki wake wote wakiwemo wakongwe katika muziki wa Dansi Nchini Maalimu Gulumo ' Kamanda' Saidi Mabela ' Dkt. Mabela' na wengine wote watafanya vitu vyao siku hiyo kwa ajili ya kukonga nyoyo za mashabiki wao wa Masasi Aliongeza Super D

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad