HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, May 18, 2012

Mjue Mwanalibeneke Dogo Kuliko Wote Duniani

Gloson, 10 Years Old
Gloson, 10 Years Old

Na Pius Micky wa Libeneke la Spoti Starehe.
 
Jina Gloson kwa Malaysia limekuwa si geni kwenye vyombo vya habari hasa baada ya kuandikwa sana kw mwaka jana namaanisha nusu ya mwisho ya mwaka jana. 

Gloson ni mtoto wa miaka 10 lakini ni Blogger anayekuja kwa kasi akiwa na miezi si zaidi ya saba kwenye ulimwengu huu wa magazeti tando, Kipaji chake si tu kwa kublog bali ni uwezo mkubwa alionao wa kujieleza, mara ya kwanza nilisoma kwenye gazeti la The Star haikuniingia hadi nilipoona akihojiwa kwenye Chanel kubwa ya Tv3 na kumuona kwa macho yangu. 

Dogo anakipaji kweli kweli na ye anasema ana blog kila kitu anachoona kina manufaa kwa jamii na katika blog yake pia amefundisha jinsi ya kuandika Post yenye mvuto na jinsi ya kuchangia topic bila kwenda nje ya mada, akiwa ni wanafunzi wa shule ya msingi Gloson anasema alipata wazo la Ku blog toka kwa mama yake ambaye alimshauri ablog naye akaanza. 

Mbali na kipaji hicho pia Gloson anakipaji cha kuandika mashairi akiwa meshaandika zaidi ya mashairi 100 ambayo yamechapishwa www.poetrytalents.com
Ikiwa na miezi 6 tu tangu ianzishwe blog ya Gloson ambayo inakwenda kwa anuani ya http://www.glosonblog.com/
Nafurahi ninapo share nilichojifunza na wenzangu
“Nafurahi ninapo share nilichojifunza na wenzangu”
 
“naamini nina mchango kwa jamii mengi waweza kujifunza toka kwangu na kuelimika, kuna mengi yakujifunza kwenye mtandao, napenda Internet naweza kufanya kila kitu kuanzia Homework, games, kununua vitu na kuwasiliana na vitu, alisema Gloson alipohojiwa kwenye Tv3. 

“kuna vitu siwezi kuwaeleza wazazi wangu moja kwa moja lakini huwa natuma email na naenda kulala nikiamka baba atanijibu ama kwa email au hata akikaa kimya najua anatafakari na amepata ujumbe wangu” aliongeza mtoto huyu anayejua kujieleza kwa lugha ya ufasaha na kufanya wtangazaji wote kucheka. 

Pamoja na vipaji hivyo pia Gloson anakipaji cha kutumia Photoshop kwa ajili ya kucheza na picha, na ni mtundu wa mambo ya mtandao pia.
Si mbaya mtembelee hapa utakuta mengi sana ya kujifunza toka kwake. Wana Blog wenzangu mpooo!!!!?

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad