HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, May 29, 2012

Martin Sospeter awa Meneja Mpya wa Bendi ya Mashujaa baada ya Kuondoka Twanga Pepeta

Meneja mpya wa bendi ya Mashujaa Martin Sospeter (katikati) akizungumza na waandishi wa habari wakati akitangaza kujiunga na bendi hiyo kwenye ukumbi wa Busness Kijitonyama asubuhi hii.Kulia ni King Dodoo ambaye ni Kaimu Meneja wa bendi ya Mashujaa na Kushoto ni Kiongozi wa Bendi hiyo,Charles Baba.Picha na Full Shangwe Blog.

Ifuatayo ni Taarifa ya Meneja huyo Mpya wa Bendi ya Mashujaa.

"Juzi usiku nilishangazwa na kauli ya mkurugenzi wangu wa zamani katika Bendi ya African Stars,Asha Baraka katika vyombo mbalimbali vya habari kuwa amenifukuza kazi kutokana kuhujumu bendi ikiwemo kushawishi wanamuziki kujiunga na bendi ya Mashujaa.

Kwa kweli kauli ile ilinisikitisha sana kutokana na ukweli kwamba Asha nilimchukulia kama dada yangu,kwani nilifanya naye kazi kwa miaka 14 iweje hii leo aje anitolee maneno ya kunichafua katika vyombo vya habari?

Mimi sijawahi kuhusika na mpango wowote wa wasanii wa Twanga kuhamia Mashujaa na wala sikuwa nafahamu mpango huo zaidi ya mwisho wa siku kusikia fununu za chinichini na mwishowe wasanii hao kutangazwa kuhamia Mashujaa.


Leo napenda nitangaze rasmi kwamba nimeachana na African Stars na kujunga na Mashujaa Entertainment na tayari nimeshasaini mkataba wa kazi katika bendi hii".

“Nilipanga nifanye taratibu za kumuaga kutokana na kuwa nilikuwa nafanya kazi kwake bila ya mkataba lakini nimepata bendi hii ambayo tulikaa na kukubaliana mambo mbalimbali.

Mbali na mkataba baadhi ya makubaliano na uongozi wa mashujaa ni pamoja na kunipangia nyumba hali itakayoniladhimu kuhama ile iliyokuwa chini ya Twanga.

Ninaamini nitafanya vema kazi yangu hii mpya kama ilivyokuwa Twanga ambapo nilidumu kwa muda mrefu na kuchangia kufika hadi hapo nilipoachia, hivyo naomba ushirikiano kwa uongozi, wanamuziki, Wadau na hata ninyi mwaandishi wa habari"Mwisho wa taarifa.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad