Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,akiwahutubia wageni waalikwa na wanachama wa CCM, waliohudhuria katika hafla ya uzinduzi wa vitabu viwili vya Binadamu na Kazi na Ukweli kwa mujibu wa Biblia, na Kurani Tukufu,Suna za Mtume na Sheria za nchi, vilivyotungwa na Katibu Mkuu Mstaafu wa Chama cha Mapinduzi CCM, Yusuph Makamba. Hafla hiyo imefanyika leo katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam, imefanyika sambamba na hafla ya kumpongeza kwa kuitumikia nafasi yake ya Katibu Mkuu wa CCM hadi anastaafu.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,akionyesha Kitabu cha Ukweli kwa Mujibu wa Biblia, Kuran Tukufu, Suna za Mtume na Sheria za Nchi, baada ya kukizindua kitabu hicho kilichotungwa na Katibu Mkuu Mstaafu wa Chama cha Mapinduzi CCM, Yusuph Makamba (kulia) wakati ya uzinduzi huo uliofanyika kwenye ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam leo,sambamba na hafla ya kumpongeza kwa kuitumikia nafasi yake ya Katibu Mkuu wa CCM hadi anastaafu. Kushoto ni Mke wa katibu huyo, Mama Makamba.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,akizungumza jambo na Katibu Mkuu Mstaafu wa CCM, Yusuph Makamba, wakati wakiwa katika hafla ya uzinduzi wa vitabu vya Ukweli kwa Mujibu wa Biblia, Kuran Tukufu, Suna za Mtume na Sheria za Nchi na Binadam na kazi,vilivyotungwa na Katibu huyo. Uzinduzi huo umefanyika leo kwenye Ukumbi wa Karimjee Dar es Salaam.
Baadhi ya wageni waalikwa waliohudhuria hafla hiyo.Picha na Muhidin Sufiani-OMR.







No comments:
Post a Comment