HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, May 30, 2012

Jeshi la polisi laanzisha dawati la watoto na jinsia mkoani Kilimanjaro

Balozi wa UNICEF afrika ambaye pia ni mwanamuziki nguli kutoka Zimbabwe Oliver Mtukudzi akizungumza wakati wa uzinduzi wa dawati la watoto na jinsia uliofanyika katika vituo vya polisi vya mjini Moshi na wilayani Hai.
Mgeni rasmi DCI Robert Manumba akiongoza wageni wengine katika uzinduzi huo kucheza wimbo wa Nelia.
Mkuu wa epelelezi na makosa ya jinai nchini DCI Robert Manumba akizindua ofisi kwa ajili ya dawati la watoto na jinsia katika vituo vya Moshi na Hai.
Mkurugenzi mtendaji wa shirika la Kwieco,,ambao ni wadau wa dawati hilo Bi Elizabeth Minde akizungumza wakati wa uzinduzi wa dawati hilo.
Maofisa wa jishi la polisi wakibadilishana mawazo mara baada ya uzinduzi wa jingo hilo la Kituo cha Moshi.

Na Dixon Busagaga wa globu ya jamii Moshi.

JESHI la polisi limeanzisha dawati la watoto na jinsi kwa lengo la kushughulikia kesi zote zinahusiana na unyanyasaji wa kijinsia na ukatili dhidi ya watoto nchini kama njia moja wapo ya kuboresha utoaji wa huduma bora za ulinzi na usalama kwa raia wote na kuhakikisha vita dhidi ya vitendo vya uvunjifu wa sheria na amani vinadhibitiwa.

Hilo limebainishwa katika uzinduzi wa dawati maalum la watoto na jinsia lililofanyika katika vituo vya polisi vilivyoko katika wilaya ya Moshi na Hai mkoani Kilimanjaro.uzinduzi wa madawati haya ya kitengo cha kushughulikia unyanyasaji wa jinsia na ukatili dhidi ya watoto yalianzishwa na jeshi la polisi kwa ushirikiano wa shirika la kimataifa la watoto UNICEF ikiwa na lengo la kutoa fursa kwa kesi zinahusiana na maovu kama hayo zinashughulikiwa kwa haraka na kwa usiri mkubwa.

Akizindua ofisi hizo katika wilaya ya Moshi na Hai mkuu wa epelelezi na makosa ya jinai DCI Robert Manumba alisema jeshi la polisi limeona ni jambo la busara kutenganisha makosa ya aina hiyo na yale ya kawaida kutokana na umuhimu wao na kuongeza kwamba watoto wengi wamekuwa wakifanyia vitendo vya kikatili lakini wamekuwa wakishindwa kuyaanika kwa kuhofia siri hizo kufichuliwana hivyo kuwaingiza katika hatari zaidi.

Afande Manumba alisema jeshi la polisi pamoja na kuanzisha vitengo kama vya polisi jamii imeona kuna haja ya kuwepo dawati maalum ya kushughulikia kesi za jinsia na watoto pia alidokeza kuwa jeshi hilo likotayari kushirikiana na mtu yeyote atakayekuwa na taarifa zozote za ukatili dhidi ya watoto na kesi za unyanyasaji wa jinsia na kwamba ofisi zitafanya idadi ya ofisi katika kitengo hicho kufikia tatu baada ya kuzindua nyingine kama hiyo katika wilaya ya Temeke ya Dar es salaam.

“ katika siku za hivi karibuni kumekuwa na matukio ya ukatili dhidi ya watoto, lakini sas tatizo ambalo limekuwa likilikumba jeshi la polisi katika kushuhghulikia mashtaka haya ni uoga ulioko miongoni mwa waathirika ambao mara nyingi ni watoto na akina mama kwatumanzisha madawati haya kutatua tatizo hilo,” alisema manumba.

Wakati huohuo balozi wa UNICEF afrika ambaye pia ni mwanamuziki nguli kutoka Zimbabwe Oliver Mtukudzi alisema kwamba mtoto kama mwanadamu mwengine yeyote Yule ana haki ya kulindwa na kupewa uhuru wa kufanya kile ambacho ni bora katika ukuaji wake na kuongeza kwamba ni hatia kwa mtu yeyote Yule kuwanyanyasa, kuwanyanyapaa au kuwafanyia vitendo vya kikatili.

 Alisema kwamba kama nchi na taasisi zingine zingeiga mfano ulionyeshwa na jeshi la polisi bila shaka vitendo vya kinyama kama vile kuwaingiza watoto katika viwanja vya vita vinavyofanywa na baadhi ya nchi kama ile iliyotekea sierra leone isingetokea.

Mtukudzi alisema wao kama UNICEF wanatambua umuhimu wa kumlinda mtoto na kusisitiza serikali inapaswa kuhakikisha kwamba dawati hilo linawezeshwa ili utendaji wake wa kazi ifikie malengo na matarajio ya wananchi hasa watoto na wanawake ambao ndio mara wamekuwa wahanga wakubwa wa matukio kama hayo. alisema kutokana na takwimu za hivi karibuni zaidi ya 70% ya watoto wamejikuta katika matukio ya kikatili lakini ni wachache ndio wamepata fursa ya kesi zao kushughulikiwa.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad