HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, May 28, 2012

Bonanza la Wauguzi wa Hospitali ya Muhimbili lafana sana

Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili akifungua Bonanza la Michezo Muhimbili lililofanyika Viwanja vya Posta Kijitonyama mwishoni mwa juma.
Mchezaji toka timu ya mpira wa pete Kurugenzi ya Tiba Shirikishi akichukua kikombe toka kwa Mkurugenzi Mtendaji, Dkt. Marina Njelekela.
Mchezaji wa mpira wa miguu akipokea kikombe cha Ushindi wa mpira wa miguu Kurugenzi ya Uuguzi.
Mshiriki wa kuvuta kamba wanaume kutoka Kurugenzi ya Ufundi akichukua kikombe cha ushindi.
Mshiriki kuvuta kamba wanawake, Kurugenzi ya Uuguzi akichukua kikombe cha ushindi.
Mshindi riadha mita 100 kutoka Kurugenzi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiiano akichukua bahasha yenye kitita ambacho ni siri yake
Picha ya pamoja na kati ya waliotwaa vikombe na Mkurugenzi Mtendaji Dkt. Marina Njelekela wa tatu kutoka kulia, akifuatiwa na Dkt. Raymond Mwenesano, Mwenyekiti Kamati ya Michezo,Mkurugenzi wa Ufundi Eng. Gaudence Aksante, , Mkurugenzi wa Utumishi Bw. Makwaia Makani na aliyeko mkono wa kulia wa Dkt. Njelekela ni Mkurugenzi wa Tiba Shirikishi Dkt. Praxeda Ogweyo.

Kurugenzi ya Uuguzi imezichachafya Kurugenzi nyingine za Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa kutwaa Vikombe viwili vya ushindi huku ikiongoza katika mpira wa miguu na kuvuta kamba wanawake katika Bonanza la Michezo lililofanyika Jumamosi iliyopita Viwanja vya Posta Kijitonyama.

Uuguzi ilichukua vikombe hivyo baada ya kuingia fainali katika mchezo wa mpira wa miguu kati yake na Kurugenzi ya Ufundi ambapo hadi kipindi cha pili, Ufundi walitandwika bao moja kwa sufuri. Upande wa kuvuta kamba wanawake Uuguzi iliibuka kidedea baada ya kuiangusha Kurugenzi ya Ufundi na hivyo kuchukua vikombe viwili.

Kurugenzi ya Ufundi ilishinda kuvuta kamba wanaume kwa kuwatoa kimasomaso Kurugenzi ya Uuguzi ambapo Kurugenzi ya Tiba Shirikishi iliibuka kidedea katika mpira wa pete kwa kuitandika Timu ya Uuguzi.

Katika riadha, Kurugenzi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano nayo ilichukua ushindi kwa mshindi wa kwanza na wa pili ambapo katika mchezo wa kufukuza kuku Mkurugenzi wa Utumishi Bw. Makwaia Makani alijitwalia kitoweo hicho kwa upande wa wanaume na Sr. Salome Mayenga alijitwalia pia kitoweo na kuifanya siku ya jumamosi kuwa njema baada ya kuondoka na kuku hao ambao kila mmoja alikadiriwa kuwa na uzito usiopungua kilo mbili. Katika michunao hiyo Kurugenzi ya Upasuaji, Tiba na Utumishi ziliondoka mikono mitupu.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad