HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, November 11, 2011

vurugu za Mwanjelwa mbeya leo,hali bado ni tete

Askari Polisi wakijalibu Kutuliza Ghasia katika eneo la Mwanjelwa jijini Mbeya wakati wa kuwatawanyisha Wamachinga waliokuwa wameanzisha vurugu leo.hali bado ni tete jijini humo mpaka hivi sasa na inasadikiwa kuwa watu kadhaa wamepoteza maisha na wengine kujeruhiwa.
Baadhi ya Wamachinga wa jijini Mbeya wakiwa Tayali kwa ajili ya Kupambana na Askari Polisi kikosi cha FFU wakati wa tukio hilo leo.Wamachinga hao wamefika katika ofisi za Watendaji wa Kata ya Sinde na ile ya Uyole na kuziharibu haribu ofisi hizo kwa madai kwamba hazina sababu ya kuwepo,kwani wao wanataabishwa kwa sababu ya watendaji hao.
Baadhi ya Wamachinga Mbali mbali wakikimbia katika eneo la tukio wakati machafuko hayo yamepamba moto.
Baadhi ya wananchi wakiwa wameokoka katika eneo hilo.
Watu Mbali Mbali wakiwa wanakimbia ili kujiokoa na Hatari katika eneo hilo.Picha na Latest News Blog.

1 comment:

  1. HAYA SASA KUMEPAMBA MOTO WANANCHI HAWATAKI KUTAWALIKA UNADHANI ITAKUWAJEEEEE! nway POLENI MACHIZI WANGU WA MBEYA!

    ReplyDelete

Post Bottom Ad