HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, November 16, 2011

MJANE MKOANI TANGA ANYANYASWA NA DIWANI ALIEMALIZA MUDA WAKE

MJANE ELIZABETH NYELLO WA KJIJI CHA BAGHAI WILAYANI LUSHOTO MKOA WA TANGA AKIWA KATIKA TAFAKARI MARA BAADA YA DIWANI ALIYEMALIZA MUDA WAKE KUTUMIA MADARAKA YAKE YA AWALI YA KUSHAWISHI WATU KUHARIBU MAZAO YAKE KWA KUPITISHA BARABARA SHAMBANI KWAKE BILA KUPEWA TAARIFA YEYE WALA UONGOZI ULIOPO MADARAKANI HIVI SASA.

Na Gift Mark- Tanga

Wakati Serikali ikiwa mbioni kutetea wajane Diwani wa zamani wa chama cha Mapinduzi (CCM) Ramadhani Mdimu wa kata ya vuga kijiji cha Baghai wilayani Lushoto anadaiwa kuvamia shamba la mjane na kufanya uharibifu wa mimea iliyopo shambani hapo kwa nia ya kupitisha barabara kwa lazima bila kufuata utaratibu na sheria za uchimbaji wa barabara.

Katika hali ya unyanyasaji uliokithili kiongozi huyo wa zamani aliyemaliza muda wake alifanikiwa kushawishi majirani zake na kuwaamuru watu hao kukata mimea ikiwemo migomba,kahawa,maharage na miti ya matunda na hatimaye kuchimba barabara kwa kutumia madaraka yake aliyokuwa nayo hapo awali.

Akiongea na Ripota Wetu Mwenyekiti wa kijiji Mahimbo Shenyange amesema baada ya kupata taarifa juu ya tukio hilo alifika eneo la tukio na kukuta migomba imekatwa katika eneo hilo kwa madai kuwa wanataka kupitisha barabara.

Mwenyekiti huyo alitoatamko la kusimamisha uchimbaji huo wa barabara akidai hanataarifa yeyote juu ya utendaji wa swala hilo wala hakuna kikao walichokaa kwa ajili ya kujadili suala hilo bali ni watu wachache waliochukua maamuzi yakutekeleza haja zao binafsi.

“Baada ya kusikia kunawatu wanachimba barabara hapa shambani nilifika eneo la tukio na kuwasimamisha wasiendelee na zoezi hilo hadi pale serikali ya kijiji itakapo waruhusu, chakushangaza walianza kunishambulia kwa maneno na kudai kuwa hawautambui uongozi wa Serikali iliyopo madarakani, wakati wanatamka hayo sikutaka kushuhudia uharibifu huo wa mazao kwa makusudi niliamua kuondoka nikawacha hapo shambani”, alisema Mahimbo.

Mmiliki wa shamba hilo Elizabeth Nyello amesema mwaka jana Mdimu na wenzake walimharibia mazao yake kwa nia ya kupitisha barabara yeye akiwa ni mgonjwa amelazwa hospitalini jijini Dar es salaam ambapo suala hilo alilipeleka ngazi ya wilaya katika dawati la unyanyasaji lililopo chini ya jeshi la polisi Lushoto.

Bi Elizabeth alisema Polisi wanaoendesha dawati hilo walimwita Mdimu na kufanikiwa kusimamisha zoezi hilo, baada ya aliyekuwa mkuu wa kituo hicho kuhamishwa na afande wa dawati la unyanyasaji kwenda masomoni, diwani huyo wa zamani alilifufua zoezi la uchimbaji wa barabara katika shamba hilo kwa kasi kubwa.

“ Kama wanyonge wanatafuta msaada Serilikalini mimi nikimbilie wapi, kijana hana utu wala ubinadamu kabisa! sasa niende wapi mimi mjane? tangu mwaka 76 namiliki shamba hili ambalo limekuza na kuwasomesha watoto wangu lakini sasa wanataka kuniua mimi na watoto wangu kwa ajili ya shamba langu, napata vitisho vingi, matusi makubwa pamoja na uharibifu wa mali zangu wanyonge tukimbilie wapi” alisema bi Elizabeth huku machozi yakitiririka.

Aidha mmiliki wa shamba hilo ameongeza kusema Mdimu na wenzake wanaunda mbinu ya kutoka kuwabambikia kesi watoto wake na kuongeza kuwa wamepanga safu ya mashahidi wao wa uongo ilikuwagandamiza watoto hao ambao wanajitokeza kutetea haki ya shamba hilo, ambapo wameonekana mara kwa mara wakienda kituo cha polisi Lushoto kupeleka maelezo ambayo hayohusiani na kesi ya msingi iliyofunguliwa kituono hapo.

Sanjari na hilo bi Elizabeth ameonyesha wasiwasi wake na kusema mapambano yake na Mdimu hayataishia hapo kwani ameahidi baada ya kukamilika kwa sakata la barabara anatarajia kujenga Msikiti katika shamba la bi Elizabeth ambalo ameuziwa na ndugu zake Mdimu lililoko mpakani mwa kijiji cha Kwemkuyu alipozaliwa Mdimu,

Juhudi za uharibifu wa mazao na lugha za matusi zilishamiri hali iliyowapelekea watoto wa mjane huyo kutoa taarifa polisi, ambapo polisi walifika eneo la tukio na kutoa tamko la kusimamisha uchimbaji wa barabara hiyo lakini watu hao walipuuza amri ya Serikali na kuendelea kuchimba.

Mkuu wa kituo cha polisi wilayani Lushoto Afande Joseph amethibitisha kutokea kwa tukio hilo, wakati akiongea na gazeti hili kwa njia ya simu na kuongeza kuwa ametuma askari wake eneo la tukio na kukuta uharibifu wa mazao.

“Baada ya kupata taarifa hiyo nilituma askari wangu kwenda eneo la tukio na baada ya kufika huko walikuta migomba 29 imekatwa pamoja na uharibifu wa mazao mengine.” alisema mkuu wa kituo cha polisi Lushoto.

Kwa upande wake Diwani aliyepo madarakani Hashim Ally Shechonge amesema amefika shambani hapo na bwana shmaba ili kutathmini uhalibifu uliojitokeza na kujua thamani yake.

Shechonge amelaani kitendo hicho na kusema kuwa licha ya unyanyasaji unaofanyika kitendo hicho kinadalili ya kuigawanya jamii na kusisitiza kuwa uchimbaji wa barabara hufuata utaratibu kuanzia ngazi ya kijiji, kata, tarafa na wilaya chini ya usimamizi wa mamlaka husika lakini watu hao walichukua madaraka wenyewe bila kujali kuwa ipo serikali katika eneo hilo.

Hatua ya bw.Mdimu ya kutoutambua ungozi ulioko madaraka na kufanya maamuzi ya vitendo vinavyo hatarisha amani ya nchi, imepelekea uongozi wa kijiji hicho kuweka kikao na viongozi wa ngazi za juu ili kujadili suala hilo ikiwa ni pamoja na mjumbe kutoka ofisi ya mbunge wa Lushoto na juhudi za kumpata mlalamikiwa ziligonga mwamba.

Kwa mujibu wa maelezo ya mkuu wa kituo cha Lushoto amesema kesi hiyo inatarajiwa kufikishwa mahakamani punde tu upelelezi utakapo kamilika, na watu wanaoshikiliwa na jeshi hilo la polisi kuhusika na tuhuma hizo ni Ramadhani Mdimu na Shabani Omari, watuhumiwa wote wapo nje kwa dhamana.

Kwa mara ya mwisho gazeti hili lilipoongea na mkuu wa kituo hicho cha polisi Lushoto alisema bwana shamba waliye mtuma kuaangalia tathimini ya uhalibifu amekaimilisha kazi yake hatua inayofuata nikujua kiasi cha fidia atakayolipwa mwadhilika wa tukio hilo, swali la kujiuliza ni kwamba maamuzi ya fidia yanatolewa na jeshi la polisi au mahakama, katika kesi ya kuingia kwa jinai.

Nivema jeshi la polisi likachukua hatua za makusudi ili kunusuru maisha ya mama huyo na familia yake kutokana na kupewa vitisho na watoto wake kutoishi kwa amani kutokana na watu hao kila kukicha kutafuta mbinu mbadala ya kutaka kuwasweka ndani.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad