HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, November 14, 2011

MAFURIKO UWANJA WA NDEGE MWANZA YASABABISHA UWANJA KUFUNGWA KWA MUDA, ABIRIA WASHINDWA KUSAFIRI

Mvua kubwa iliyonyesha leo jijini Mwanza kwa takribani masaa manne bila kupumzika imeathiri kwa kiasi kikubwa shughuli za usafirishaji kwa njia ya anga kutokana na maji mengi kujaa katika uwanja wa ndege wa jijini humo.kama ionekanavyo pichani hapa.
Ngazi Maalum zinazotumika kapandia abiria kwenye ndege kama zinavyoonekana kutokana na mafuriko yaliyoikumba airport ya jijini Mwanza leo mara baara ya mvua kubwa kunyesha.
Hakuna Ndege yeyote iliyoondoka wala kutua leo jijini Mwanza maana hali ilikuwa ni mbaya sana.
Hapa leo hakukuwa na kazi yoyote nyingine leo.
Sehemu ya kurukia Ndege ikiwa imeharibika vibaya kutokana na Maji ya Mvua iliyonyesha siku ya leo Jijini Mwanza.
Wafanyakazi wa Kiwanja cha Ndege cha Mwanza wakiendelea kufanya taratibu ya kuweka vitu sawa katika chumba cha kupita abiria wanaosafiri.huku maji yakiwa yameingia mpaka ndani.
Ndege zilizofanikiwa kuruka katika uwanja huo wa Mwanza ni hizi tu,lakini zile za abiria hakuna hata moja iliyoweza kuondoka wala kutua.
Wafanyakazi mbalimbali wa kiwanja cha Ndege cha Jijini Mwanza wakishughulika kusafisha njia za ndege mara baada ya magugu na tope jingi kutanda katika eneo hilo.
Ilikuwa ni kama bahari ndogo katika kiwanja cha Ndege cha Jijini Mwanza leo.Picha Zote na Mdau G Sengo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad