Mratibu wa Kinga ya Ukimwi wa Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma, Peres Kamugisha (kulia) akipokea mwenge kutoka kwa mmoja wa wakimbiza mwenge kitaifa mwaka huu,Elisha Lawrence Gama,mara baada ya kuwasili wilayani humo hivi karibuni.
Mkimbiza Mwenge kitaifa mwana huu,Elisha Lawrence Gama akitoa ujumbe wa mwenge kwa wananchi wa Wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma katika viwanja vya CCM wilayani humo.
Kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa,Bi Mtumwa Rashid Alfani akijiandaa kumpa tone la vitamini A mtoto wa miaka 2 Athumani Idd baada ya kuzindua zoezi la chanjo kwa watoto walio chini ya umri wa miaka mitano wilayani Namtumbo hivi karibuni.
Kiongozi wa mbio za Mwenge kitaifa,Bi Mtumwa Rashid Alfani akimpatia tone la vitamini A mtoto Suzy Lucas Njela ikiwa ni ishara ya ufunguzi wa zoezi la chanjo kwa watoto walio na umri chini ya miaka mitano katika wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma hivi karibuni,ambapo Wilaya hiyo imekusudia kutoa chanjo ya magonjwa mbalimbali kwa watoto zaidi ya 143,133 kiwango ambacho ni kikubwa ikilinganishwa na wilaya zingine za mkoa huo.Picha na Muhidini Amri.
No comments:
Post a Comment