HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, October 7, 2011

Tancut Almasi Orchestra na Kashasha

Na Mzee John Kitime

Kuanzia album ya kwanza ya Tancut Almasi Orchestra , bendi iliendelea kutoa vibao vilivyoweza kudumu katika kumbukumbu za wote waliovizisikia kuanzia enzi hizo, album ya kwanza ilikuwa na nyimbo kama vile, Nimemkaribisha nyoka(Kasaloo Kyanga), Kashasha(Kyanga Songa), Tutasele (Kasaloo), Mtaulage(John Kitime), Big Four(Utunzi wa wimbo huu ulileta utata kwani ulianza kwa ugomvi kwa Mamado Kanjanika kudai kuwa aliutunga yeye wakati akina Kasaloo na Kyanga wakidai wameutunga wao. Lakini hatimae akina Kasaloo waliacha ugomvi huo na Mamado hutajwa kama mtunzi wa wimbo huu. 

Hebu angalia mambo yalivyokuwa wakati Kashasha likipigwa. Niko hapo na miwani kubwa nikiungurumisha rhythm guitar.

Kwa habari zaidi za muziki wetu,Bofya Hapa.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad