HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, September 1, 2011

Warembo Vodacom Miss Tanzania kuchuana kutafuta mrembo mwenye vipaji jumamosi hii

Na Mroki Mroki

Warembo 30 wanaowania taji la Vodacom Miss Tanznia 2011, wanataraji kupanda jukwaani kuchuana vikali katika shindano la kumtafuta mrembo mwenye kipaji (Miss Talent 2011) shindano litakalo fanyika Jumamosi Septemba 3,2011 katika Hoteli ya Kitalii ya Giraffe Ocean View iliyopo Mbezi Beach jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaaam leo, Mkuu wa Itifaki wa Kamati ya Miss Tanzania, Albert Makoye alisema shindano hilo litakuwa kali na lakuvutia hasa kutokana na warembo wa mwaka huu
kuonesha uwezo mkubwa wa vipaji katika vitu mbalimbali.

“Shindano litakuwa zuri sana na la ushindani mkubwa maana kwanza warembo wanatafuta tiketi ya kuingia nusu fainali na pia kutafuta taji miongoni mwa warembo hao 30, wa mawaka huu,”alisema Makoye.

Warembo hao wa Vodacom Miss Tanzania 2011, wanataraji kuonyesha vipaji vyao mbalimbali katika shindano hilo ambapo mshindi atajipatia tiketi ya kuingia Nusu fainali ya Shindano la Vodacom Miss Tanzania.

Warembo hao wataoneshana umwamba wa vipaji vyao katika uimbaji, kucheza mziki wa aina mbali mbali na aina nyingine za vipaji binafsi walivyonavyo washiriki hao. Nao warembo Jeniffa Kakokali, Rose Albert, Dallilah Ghalib kwa nyakati tofauti wamesema wamejiandaa vya kutosha kuonesha vipaji vyao katika kucheza na kuimba.

Kingilio katika shindano hilo litakalopambwa na burudani kali kutoka kundi machachari la burudani la THT itakuwa ni Tsh 10,000/= huku Mgeni rasmi akiwa ni mwanamitindo wa kimataifa Cynthia Kanema ambaye pia aliwahi kuwa Miss Zambia 2003 na anafanyashughuli zake za mitindo katika nchi za Italy na Uingereza.

Tayari warembo wa tatu wameshajikatia tiketi ya kuingia nusu fainali ya Vodacom Miss Tanzania kwa kushinda mataji ya Top Model lililokwenmda kwa Mwajabu Juma, Miss Photogenic lilinyakuliwa na Tracy Mabula na Miss Sport Lady lililokwenda kwa Loveness Flavian.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad