SHIRIKA
la utangazaji la Ujerumani (Deutsche Welle) Limeendelea kuimarisha
huduma zake nchini Tanzania kwa kuungana na Vodacom Tanzania kwa kurusha
kipindi cha ‘Learning by Ear” kwa njia ya simu.
Kuanzia
Septemba nane mwaka huu, hadithi fupi maarufu ya redio inayorushwa na
DW, inayojulikana kama “Learning by Ear”, itapatikana kwa mahitaji kwa
watumiaji wa huduma za simu.
Programu
hii inawalenga vijana ambapo inatoa elimu juu ya masuala ya UKIMWI,
haki za binadamu, demokrasia, na mazingira ikiambatana na simulizi na
makala mchanganyiko za kisisimua na kuburudisha.
Learning
by Ear inatolewa katika luga zote zinazotumika katika programu za radio
hiyo inayolenga wasikilizaji wa kiafrika. Tayari inarushwa hapa
Tanzania kama majawapoza programu za DW-RADIO/Kiswahili.
Deutsche
Welle’s kwa Kiswahili ni kati za programu za radio hapa nchini, ambapo
inakadiriwa kuwa takiriban silimia 70 ya watanzania wanafahamu Deutsche
Welle radio na kila theluthi moja ni msikilizaji wa mara kwa mara wa
programu za Kiswahili zinazo rushwa na radio hii.
Mbali
na kurusha matangazo yake kwa luga ya Kiswahili, radio hii pia hutoa
habari kwa njia ya ujumbe fupi (sms-news) za kila siku kupitia simu za
mkononi, tovuti iliyosheheni habari nyingi muhimu
(www.dw-world.de/kiswahili), mtandao wa kijamii kama Twitter na
Facebook.
Wateja
wa Vodacom ambao wamejiunga na huduma ya “Music Radio”, kutoka Vodacom
Tanzania, wanaweza wakapata sehemu zote za kipindi cha “Learning by Ear”
kwa bei ya kipekee itakayotegemea matumizi kwa sekunde.
Wateja
watatakiwa kupiga namba 09011 22 201 kwenye simu zao ili kupata huduma
ya ‘music services’ na watatakiwa kusikiliza maelekezo ya namna ya
kupata mitiririko mbalimbali ya vipindi cha ‘Learning by Ear ’.
Learning
by Ear ilianzishwa kama kipindi cha Deutsche Welle mwaka 2008 kwa
Afrika, kwa ushirikiano na Ofisi ya kimataifa ya mambo ya nje ya
Ujerumani, na ni moja ya vipindi vilivyofanikiwa sana kwa wasikilizaji
vijana.
Kipindi
hicho kwa sasa kinazalishwa kwa ushirikiano na marafiki walioko Afrika
na kuandikwa na Wahariri wa kiafrika. Zaidi ya vituo vya radio 270
kutoka Nchi mbalimbali za Afrika zinarusha kipindi hicho tangu
kianzishwe mwaka 2008, na kukifanya kupata tunzo nyingi ikiwamo ile ya
‘kipindi chenye ubunifu wa juu kwa Radio’ ya mwaka 2009 kutoka Chama cha
Kimataifa cha Utangazaji(AIB).
Deutsche
Welle ni kituo cha utangazaji cha Ujerumani,ikiwa na vituo kama DW-TV,
DW-RADIO na DW-WORLD.DE, zote zikiwa zinazalisha habari, kuangalia
tamaduni mbalimbali duniani kote na kuandaa midaalo ya kubadilishana
tamaduni.
Vodacom
Tanzania Ltd ni kampuni ya mtandao wa simu inayotoa huduma za
mawasiliano ya GSM kwa wateja zaidi ya milioni 9 nchi nzima kwa sasa.
Hivi
karibuni Vodacom ilizindua huduma ya haraka ya Radio na Tv kwa njia ya
simu, kwa kutumia mtandao mpana ilionao nchi nzima na bado kampuni
inaendelea na tafiti kwa ajili ya huduma zitakazowanufaisha watanzania
zaidi.
No comments:
Post a Comment