HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, August 31, 2011

REDDS KUANDAA ONYESHO KUBWA LA MAVAZI NA WASHIRIKI WA MISS TANZANIA 2011 KUSHEHEREKEA MIAKA 50 YA UHURU

Redds Miss Kinondoni 2011, Stella Mbuge akimpatia zawadi mama aliyejifungua muda mfupi katika hospitali ya Mwananyamala wakati warembo hao waliopo katika kambi ya Miss Tanzania walipotembelea hospitali hiyo na kutoa zawadi ya Iddi.Warembo hawa watashiriki onyesho kubwa la mavazi litakalofanyika hivi karibuni.
Redds Miss Ilala 2011,Salha Israel akiwa na mama aliyejifungua katika hospitali ya mwananyamala wakati warembo hao waliopo katika kambi ya Vodacom Miss Tanzania walipoenda kuwatembelea na kutoa zawadi ya Iddi.Warembo hawa watashiriki onyesho kubwa la mavazi litakalofanyika hivi karibuni.

Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia kinywaji chake cha Redd’s Original imeandaa maonesho makubwa ya mavazi yatakayowashirikisha warembo wa Miss Tanzania 2011 kuadhimisha miaka 50 ya uhuru wa Tanzania.

Redd’s ambayo ni kinywaji rasmi cha shindano la Miss Tanzania 2011 wamedhamiria kutumia maonesho haya kama chachu ya kuwapatia washiriki nafasi ya kuonesha vipaji vyao katika sanaa ya mitindo.na kuwakutanisha na wadau wa fani ya mitindo ili waweze kujipatia njia mbadala ya kujiendeleza baada ya mashindano.

Akiwa anaongea kuhusiana na onesho hili meneja wa kinywaji cha Redds Bi. Victoria Kimaro alisema “Redds kama mdhamini aliyeshiriki kikamilifu kwenye mashindano haya ya urembo toka kwenye ngazi za chini za vitongoji imetambua kuwa kuna umuhimu wa kuwapatia washiriki nafasi za ziada za kuonesha vipaji vyao kwenye fani mbalimbali ikiwemo ya ulimbwende na mitindo ili kuwawezesha kuwa na njia mbalimbali za kujipatia mafanikio ya kimaisha. 

Maonesho haya ya mavazi yatawakutanisha warembo na wadau mbalimbali wa mitindo kama wabunifu wa mavazi, taasisi za walimbwende na makampuni ya matangazo ili waweze kugundua vipaji vipya na kuvipatia nafasi ya kuviendeleza.”

 Bi. Kimaro aliendelea kwa kusema kuwa “Tasnia ya urembo ina mchango mkubwa kwenye jamii yetu sio tu kwa upande wa burudani bali inawapatia nafasi warembo mbalimbali Tanzania kukuza vipaji vyao na kuwekea msingi ambao wakijipanga vizuri utawajenga na kuwaletea mafanikio mbalimbali kweye maisha yao. 

 Maonesho haya ya mavazi ni mojawapo ya fursa ambayo Redds inayowapatia warembo wakuze vipaji vyao kama njia mbadala ya kujipatia maendeleo na mafanikio baada ya shindano la kitaifa.”

Maonesho hayo ambayo yatafanyika siku ya Ijumaa ya tarehe 2 Mwezi wa 8 katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam yatajumuisha wadau mbalimbali wa mitindo, burudani kutoka kwa Banana Zorro na B Band pamoja na mwanadada mkali wa mziki wa kizazi kipya Shaa.

Warembo wa Miss Tanzania siku ya onyesho watavaa nguo zilizobuniwa na wanamitindo mbalimbali kama Binti Africa,, Kijo na Franco.

Onyesho hili pia limemshirikisha mwanamitindo maarufu kutoka mji wa New York ambaye pia amefanya kazi na wabunifu mbalimbali wa kimataifa na nyota mbalimbali wa nchini Marekani Bi. Rosemary Kokuhilwa ajulikanaye kama Fashion Junkii.

Siku ya onesho warembo wataanza na safari ya kutembelea kiwanda cha Bia Tanzania (TBL) kilichopo Ilala Dar es Salaam ambapo watashuhudia mtiririko mzima wa upikaji wa bia na kujumuika na wafanyakazi wa kiwandani hapo kwenye chakula cha mchana.

Redd’s Original imeshiriki kikamilifu kwenye mashindano ya Miss Tanzania 2011 ambapo imefadhili zaidi ya vitongoji 35 na pia kama mdhamini mkuu wa Redds Miss Ilala, Redds Miss Temeke na Redds Miss Kinondoni.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad